HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, April 1, 2023

TGNP, CHUO CHA COADY CANADA WATOA MAFUNZO JUU YA UTAFUTAJI MASOKO YA BIASHARA ZA WANAWAKE

 MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) kushirikiana na Chuo cha Coady cha nchini Canada watoa mafunzo juu ya uwezeshaji kiuchumi, maisha endelevu na namna bora ya kutafuta masoko katika biashara za wanawake.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili Mosi, 2023 amesema mafunzo hayo ni ya kimataifa kwa sababu tunawashiriki kutoka India, Bangladeshi, Ethiopia, Canada na Tanzania.

Amesema kuwa wanatarajia washiriki wote watapata mbinu mpya za kutafuta masoko lakini pia kuongeza uelewa juu ya masuala ya uwezeshaji kiuchumi na maisha endelevu.

Amesema katika miradi wanayoitekeleza ipo katika nchi tano ambazo ni India, Bangladeshi, Ethiopia, Canada, Haiti na Tanzania, ingawa washiriki kutoka Haiti hawajafanikiwa kushiriki kutokana na sababu mbalimbali.

Amesema kuwa ayo ni mafunzo ya awamu ya tatu tangu wameanza ushirikiano wao na chuo cha Coady cha Canada na wanatarajia mwakani 2024 kutoa mafunzo ya kikanda yatakayohusisha wanawake na uongozi ambayo yatafanyika hapa nchini.

Amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa watu wachache ili nao waweze kutoa mafunzo hayo kwa wananchi waliopo vijijini.

“Tunaweka kipaumbele kwa watu mashina ili waweze kushiriki katika maendeleo, tukiamini kwamba watu waliopo kwenye mashina wanakuwa na uzoefu mkubwa kulingana na mazingira yao wanapoishi.

Tunaamini kwamba tukiunganisha nguvu za watu wa mashinani na watu wanaoishi mjini wote watashiriki kikamilifu kuliko wale wa vijijini wakishiriki pekeyao.” Amesema Lilian

Amesema wakiwawezesha maendeleo yatakwenda kwa haraka zaidi kuliko kuwezesha watu wanaoishi mjini kwa watu wote wanawake na wanaume, vijana na watu wenye ulemavu bila kutomuacha mtu nyuma.

Kwa upande wa mtoa mafunzo, Mfanyakazi wa Programu ya Maisha na Masoko kutoka Taasisi ya Kimataifa cha Coady, Yogesh Ghore amesema kuwa wameona fursa hapa nchini ya kuja kutoa mafunzo ya siku sita ili kumpa mwanamke ujuzi na elimu juu ya masoko ili kukuza biashara zao.

Amesema kuwa wanawake katika mafunzo hayo watafaidika kwani hapa nchini kunafursa nyingi katika maendeleo ya biashara na kilimo.

Amesema kuwa Serikali ya Tanzania wameona ipo katika kusaidia wananchi kutafuta njia tofauti ya maendeleo kiuchumi kwa wananchi.

Kwa upande wa Mshauri Elekezi wa masuala ya usawa wa kijinsia kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Hellen Urio amesema kuwa mtandao huo hawafanyikazi peke yao wanashirikiana na mashirika mengine ili kuleta sauti ya pamoja kwa sababu sauti ya pamoja huleta mabadiliko chanya.

Amesema kuwa Chuo Kikuu Cha Coady Cha Canada wamekuwa wakifanya nao kazi kwa karibu hasa katika kutoa mafunzo ya kuwawezesha wanawake ili kujikomboa kiuchumi na kuweza kujisimamia pekeyake.

Amesema TGNP imekuwa ikitoa mafunzo juu ya mwanamke kujitokeza na kugombania nafasi za uongozi.

"Lakini tunatambua kwamba mwanamke hawezi kuwania nafasi za uongozi kama hana kipato."

Akitolea mfano wa kampeni Hellen amesema kuwa Kipindi cha kampeni kinahitaji fedha nyingi hivyo lazima mwanamke awe na uchumi thabiti ili aweze kufanya kampeni bila kutegemea fedha kutoka kwa mtu mwingine.

Amesema kupitia mafunzo hayo wanatamani kumwona mwanamke sokoni kwani wanawake walio wengi wamekuwa wazalishaji mali lakini hawapo katika masoko.

Amesema mafunzo hayo pia yatamsaidia mwanamke aweze kujisimamia mwenyewe pamoja na shughuli anazozifanya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Lilian Liundi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili Mosi, 2023, kuhusiana na mafunzo ya siku sita kwa washiriki kutoka nchi tano ili nao waweze kwenda kutoa mafunzo hayo katika maeneo wanapotokea.

shauri Elekezi wa masuala ya usawa wa kijinsia kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP), Hellen Urio akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Aprili Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya washiriki wakisiliza mada leo Aprili Mosi, 2023.

Baadhi ya washiriki wakichangia mada katik mafunzo yaliyofanyika leo Aprili Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad