HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 17, 2023

TCAA YAKABIDHI VIFAA VYA OFISI KWA KITUO CHA POLISI UWANJA WA NDEGE WA MTWARA


Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA imerejesha sehemu ya faida ya mapato yake kwa jamii kwa kukabidhi vifaa vya ofisi katika Kituo cha Polisi uwanja wa ndege wa Mtwara.

Vifaa hivyo vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tano Vimekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw. Hamza S. Johari tarehe 17 April 2023 na kupokelewa na ACP Isack Mushi kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.

“Kila mwaka Mamlaka ya Usafiri wa Anga hutenga bajeti yake ya fedha kwa ajili ya Jamii inayotuzunguka (CSR). Vifaa hivi ni sehemu ya Mamlaka kurudisha sehemu yake ya faida kwa jamii inayoizunguka na tunaamini vitawawezesha Maofisa wetu kufanya kazi zao katika mazingira yaliyoboreshwa zaidi” alisema Mkurugenzi Hamza.

Akipokea vifaa hivi kwa niaba ya RPC Mtwara,ACP. Isack Mushi ameishukuru Menejimenti ya TCAA na kuahidi kuwa vitatumika kwa weledi.

“Kwa niaba ya Jeshi la Polisi nina ahidi vifaa hivi tulivyopokea leo vitatumika ipasavyo na vitatunzwa vyema kabisa. Lakini niseme wazi kuwa mahitaji bado tunayo mengi na niendelee kuwaomba milango yenu iwe wazi pindi tutakapo bisha hodi” ACP Isack Mushi.

Vifaa hivi vimetokana na ahadi iliyotolewa na Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ilipotembelea uwanja wa ndege wa Mtwara mnamo mwezi Julai, 2022 na kupata fursa ya kujiona mazingira ya uwanja huu ikiwemo mazingira ya kituo cha Polisi cha wa ndege wa Mtwara.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari (Wapili Kulia) akikabidhi vifaa vya ofisi kwa muwakilishi wa RPC Mtwara, ACP Isack Mushi. TCAA imetoa msaada wa vifaa hivi kwaajili ya Kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege Mtwara. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Teophory Mbilinyi na Wakwanza Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege Mtwara Inspekta Morgan Mlungwana.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafanyakazi wa Kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Mtwara mara baada ya kukabidhi vifaa vya ofisi ikiwa ni kurudisha kwa jamii. Kushoto ni muwakilishi wa RPC Mtwara, ACP Isack Mushi na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Teophory Mbilinyi.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Teophory Mbilinyi akizungumza jambo mara baada ya mamlaka hiyo kukabidhi vifaa vya ofisi kwenye Kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Muwakilishi wa RPC Mtwara, ACP Isack Mushi(kushoto) akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) ukiongizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari (kulia) kwa kuweza kukusaidia Kituo cha polisi cha Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza S. Johari (katikati) akiwa kwenye picha pamoja na muwakilishi wa RPC Mtwara, ACP Isack Mushi(wa pili kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka TCAA Teophory Mbilinyi(wa pili kushoto), Mkuu wa Kituo cha Polisi Uwanja wa Ndege Mtwara Inspekta Morgan Mlungwana( wa kwanza kulia) pamoja na wafanyakazi wa Kituo hicho cha polisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad