Shirika la S4C na LFS waandaa mbio za kuchangisha fedha kusaidia wasichana kupata Taulo za Kike 'Pedi' - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 12, 2023

Shirika la S4C na LFS waandaa mbio za kuchangisha fedha kusaidia wasichana kupata Taulo za Kike 'Pedi'

 

Mkurugenzi wa Smile for Community Organization (S4C), Flora Njelekela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala wakisaini hati ya makubaliano (MoU) leo kwa ajili ya kuandaa na kuratibu pamoja mbio za 'Run For Binti Marathon 2023'   ikiwa ni mkakati wa kukusanya rasilimali fedha ili kuwezesha watoto wa kike kupata taulo za kike na kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi hususani hedhi salama na safi. Wanaoshuhudia wakiwa wamesimama ni  Meneja Programu wa S4C, Aneth Kiyao (kushoto) na Meneja wa Mawasiliano LSF, Jane Matinde.

SHIRIKA la Smile for Community (S4C), kwa kushirikiana na Legal Services Facility (LSF), limeandaa mbio za "Run For Binti" kwa ajili ya kuchangisha fedha za kuwasaidia wasichana kupata taulo za kike ili kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi hususan hedhi salama.

Akizungumza na Vyombo vya habari Leo tarehe 12 Aprili 2023, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendsji wa S4C, Flora Njelekela, amesema mbio hizo zinatarajiwa kufanyika Julai, 2023, katika mikoa ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo watu takribani 1,500 wanatarajiwa kushiriki.

“Kwa mwaka huu mbio hizi zimebeba malengo maalum makuu manne, ikiwa ni pamoja na kusaidia upatikanaji wa huduma ya hedhi salama kwa wanafunzi wa kike walioko shuleni kwa kuwapa taulo za kike, kuboresha miundombinu ya shuleni ikiwemo ukarabati na ujenzi wa vyumba vya kujistiri kama vile vyoo wakati wa hedhi, utoaji wa elimu juu ya masuala mazima ya haki ya kupata hedhi salama, na mwisho ni kutoa mafunzo ya ushonaji na vifaa kwa vikundi vya akina mama ili kuweza kurahisisha upatikanaji wa taulo za kike kwa urahisi nchini," amesema Njelekela.

Amesema hii ni mara ya tatu kwa mbio hizo kuandaliwa ambapo watu zaidi ya 700 walishiriki huku fedha zilizopatikana zikipelekwa Kwa wasichana kwa ajili ya kuwanunulia taulo za kike maarufu kama Pedi.

“LSF wamekuwa moja ya wadau wakuu wa mbio hizo kwa miaka miwili sasa, hivyo tumeona vyema kuwa na ubia nao katika kuandaa na kuratibu mbio hizi ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutatua changamoto za mabinti walioko shuleni na kuhakikisha kuwa haki yao ya elimu na afya bora inapatikana.

Ushirikiano huu tunaouanza na LSF ni wa muda mrefu na makubaliano haya yatatuwezesha kuhakikisha kuwa mbio hizi zinakuwa endelevu na malengo yake yanafikiwa kikamilifu,” amesema Njelekela na kuongeza.

"Tunapenda kuwakaribisha, taasasi za kitaifa na kimataifa, makampuni, taasisi za umma, mashirika na wadau wengine wote wa maendeleo kuweza kushiriki kwa pamoja katika kufanikisha maaandalizi ya mbio hizi na hatimaye kufikia matarajio ya matokeo ya mbio kama yalivyotajwa hapo juu."

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala amesema moja ya malengo makuu ya LSF ni kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote hasa kwa wanawake na watoto wa kike, na kwamba ushirikiano kati ya shirika lake na S4C, utasaidia upatikanaji wa haki kwenye eneo la haki ya afya ya uzazi kea wasichana hususan ya kupata hedhi salama.

“Tunaratibu mbio hizi kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto ya watoto wa kike walioko shuleni kutopata haki ya kupata hedhi salama kwasababu ya changamoto mbalimbali zinazowanyima fursa ya kukabiliana na hali hiyo pindi ikiwatokea.

Takwimu zinaonesha kuwa wanafunzi wa kike hukosa masomo kwa siku 3 mpaka 4 kwa mwezi wakiwa katika siku zao na kusababisha kutofanya vizuri kwenye mitihani au hata baadhi yao kuacha shule kabisa.” ameeleza Ng’wanakilala na kuongeza:

“Tunaamini kuendelea kushirikiana na S4C katika hatua hii mpya kutatuwezesha kuboresha mbio hizi kila mwaka, kut tatuwezsha kutafuta rasilimali fedha kwa pamoja lakini pia kuweza kufikia malengo yetu makuu kwa pamoja.
Mkurugenzi wa Smile for Community Organization (S4C), Flora Njelekela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala wakionesha hati ya makubaliano waliyosaini leo kwa ajili ya kuandaa na kuratibu pamoja mbio za 'Run For Binti Marathon 2023'   ikiwa ni mkakati wa kukusanya rasilimali fedha ili kuwezesha watoto wa kike kupata taulo za kike na kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi hususani hedhi salama na safi.
Mkurugenzi wa Smile for Community Organization (S4C), Flora Njelekela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala wakisaini hati ya makubaliano (MoU) leo kwa ajili ya kuandaa na kuratibu pamoja mbio za 'Run For Binti Marathon 2023'   ikiwa ni mkakati wa kukusanya rasilimali fedha ili kuwezesha watoto wa kike kupata taulo za kike na kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi hususani hedhi salama na safi. Wanaoshuhudia wakiwa wamesimama ni  Meneja Programu wa S4C, Aneth Kiyao (kushoto) na Meneja wa Mawasiliano LSF, Jane Matinde.
Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Services Facility (LSF), Lulu Ng’wanakilala akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kuingia ubia na Smile for Community Organization (S4C) baada ya kusaini hati ya makubaliano (MoU) leo Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuandaa na kuratibu pamoja mbio za 'Run For Binti Marathon 2023' ikiwa ni mkakati wa kukusanya rasilimali fedha ili kuwezesha watoto wa kike kupata taulo za kike na kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi hususani hedhi salama na safi pamoja na kuboresha mazingira bora na rafiki katika sekta ya elimu kwa mtoto wa kike yatakayomuwezesha kupata hedhi salama kupitia ujenzi wa miundombinu bora hususani vyoo.
Mkurugenzi wa Smile For Community Organization (S4C), Flora Njelekela akiongea na waandishi wa habari wakati kutangaza kuingia ubia na Legal Services Facility (LSF) baada ya kusaini hati ya makubaliano (MoU) leo Jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuandaa na kuratibu pamoja mbio za 'Run For Binti Marathon 2023' ikiwa ni mkakati wa kukusanya rasilimali fedha ili kuwezesha watoto wa kike kupata taulo za kike na kuboresha upatikanaji wa haki ya afya ya uzazi hususani hedhi salama na safi pamoja na kuboresha mazingira bora na rafiki katika sekta ya elimu kwa mtoto wa kike yatakayomuwezesha kupata hedhi salama kupitia ujenzi wa miundombinu bora hususani vyoo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad