HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 13, 2023

PASS Trust yahamasisha wadau kuhusu ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi nchini

 



Iringa
Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS Trust) leo imefanya mkutano wa mashauriano na wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo la kuhamasisha uzalishaji unaozingatia ukuaji wa kijani shirikishi ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Gentle Hill mkoani Iringa, pamoja na mambo mengine, ulijadili njia za kuharakisha na kuimarisha maendeleo endelevu ya kiuchumi kwa kutilia mkazo Ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi kwa kilimo endelevu kitakachotosheleza mahitaji ya kujikimu, kibiashara na kuhakikisha usalama wa chakula cha uhakika na kilimo stahimilivu.

Kwa mujibu wa PASS Trust, usalama endelevu wa chakula utafikiwa kupitia mapinduzi ya kilimo yenye uthabiti na uendelevu kwa kuzingatia kanuni za Ukuaji wa Kijani Shirikishi.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Ibrahim Kaduma alisema PASS Trust ina mchango mkubwa katika kuchochea na kuwezesha ukuaji wa kilimo nchini Tanzania huku tukitoa kipaumbele kwa vijana na wanawake ambapo tunawapa dhamana ya mikopo na huduma za maendeleo ya biashara ili kufikia malengo yao”.

Akifafanua kuhusu ushirikishwaji wa wadau wengine wa kilimo katika kikao hicho, Mkurugenzi Kaduma aliongeza:

“Tunaamini katika ushirikiano na mashirika mengine yanayohudumia sekta ya kilimo, ndiyo maana tumewaalika wadau wengine wa sekta hiyo kwa ajili ya kujadili na kubainisha njia mbalimbali zinazoweza kusaidia sekta ya kilimo kupitia ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi ambayo inalenga kuhimiza ukuaji wa kilimo kwa kujali uhifadhi wa mazingira asilia”.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bi Halima Omari Dendego alitoa pongezi kwa PASS Trust juu ya kuja na mpango wa Kukuza Uchumi kupitia ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi, akisema ni njia bora ya kuchochea kilimo endelevu.

“Naipongeza PASS Trust kwa ubunifu na kuanzisha ajenda ya Ukuaji wa Kijani Shirikishi ambayo kwa hakika inachochea maendeleo endelevu ya kiuchumi ambayo yanaenda sambamba na utunzaji wa mazingira na kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo”, alisema Mkuu wa mkoa huyo na kuongeza kuwa inawawezesha wakulima kujihusisha kikamilifu na kilimo biashara kwa namna inayojumuisha jamii nzma.

Serikali ya Denmark inafadhili PASS Trust ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha na maendeleo ya biashara kwa wafanyabiashara wa kilimo nchini Tanzania, imesaidia kwa kiasi kikubwa wakulima wengi ambao wamegawanyika katika makundi matatu, ambayo ni watu binafsi, vikundi na makampuni yanayojihusisha na kilimo kupitia huduma za vifaa na misaada ya kifedha kwa ajili ya kukuza kilimobiasharag.

PASS Trust ilianzishwa mwaka 2000 kama asasi yenye lengo la kuwezesha uwekezaji na ukuaji katika kilimobiashara na sekta zinazohusiana. Hadi sasa PASS inatimiza miaka 23 tangu ilipoanzishwa huku ikiwafikia watanzania katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.

PASS inatoa huduma katika mikoa yote nchini Tanzania yenye ofisi za kanda katika mikoa sita ambayo ni Kanda ya nyanda za juu kusini (Mbeya) kanda ya kati na mashariki(Singida) kanda ya magharibi(Tabora),Kanda ya Kusini (Ruvuma),Kanda ya Kaskazini(Arusha),Kanda ya ziwa (Mwanza) na Ofisi kuu Dar es Salam.

PASS pia inapatikana kwa urahisi katika mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, YouTube, Twitter na kupitia Tovuti yenye jina la PASS Trust. Kwa maelezo zaidi inapatikana pia kwa namba ya huduma kwa wateja kwa namba ya bure 0800750037.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad