HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 17, 2023

NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI KUTIMIZA MIAKA 30 TANGU KUANZISHWA MWAKA 1993

 

















*Ngoma Africa Band aka " FFU Ughaibuni " ya Ujerumani kutimiza miaka 30 tangu kuanzishwa mwaka 1993 na kiongozi wao Kamanda Ras Makunja

Na Zainabu Ally Hamisi,
TUNAPOONGELEA tasnia ya Utamaduni ,Sanaa za maonyesho na muziki kwa upana ni tasinia inayoiwakilisha jamii,taifa katika tufe la dunia na hapa ndio pa kuitilia maanani tasinia hii na wasanii kwa ujumla wake kutokana na michango yao katka kuitangaza nchi kitaifa na kimataifa.

Mojawapo wa mabalozi wetu ni kundi la muziki la "The NGOMA AFRICA BAND' inayoongozwa na mwanamuziki mtanzania Ebrahim MakunjaKamanda Ras Makunja ambeye pia ndiye muanzilishi yeye makao yake nchini Ujerumani.

Bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi ilianzishwa 13 Augost 1993 kwa madhumuni ya kuutangaza muziki wa dansi wa Tanzania bongo dansi na miziki ya dansi ya afrika mashariki natangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 imejkuta ndio bendi pekee ya kiafrika iliyodumu kwa miaka mingi barani ulaya na kufanikiwa kuteka maelfu ya washabiki na wapenzi wa bendi hiyo amabo wenyewe mara nyngi ujigamba kwa kusema washabiki ndio wenye bendi na wanamuziki ni watumishi tu.

Ngoma Africa Band mwaka huu 2023 inatimiza miaka 30 ya kuzaliwa kwake na kufanikiwa kuuatangaza muziki wa dansi "Bongo Dansi" made in Uswahilini Tanzania kwa miaka 30 sasa. Bendi hiyo ya muziki Ngoma Africa Band ndio balozi mzuri wa kiswahili katika majukwaa ya kitamaifa kutokana na tungo za nyimbo nyingi ambazo wameziimba kiswahili kwa kupitia mtunzi wake mtata kamanda Ras Makunja "Mwenye kukaanga mbuyu".

The Ngoma Africa Band almaarufu kwa majina walibatizwa ya utani kama "FFU Ughaibuni", au Viumbe wa Ajabu "ANUNNAKI Alien's" , bendi hii imejikuta kugeuka kuwa taasisi iliyobeba na kuzalisha wanamuziki wenye vipaji vya kila aina vinavyotingisha majukwaa ya kimataifa.

Tuungane na Ngoma Africa Band katika maandalizi ya kusherekea miaka ya 30 ya kuzaliwa kwakwe na pia kuwa mabalozi wazuri wa utamaduni na muziki wetu katika majukwaa ya kimataifa kule Ughaibuni,Pia kuwa mabalozi wazuri wa lugha ya kiswahili kwa kupitia muziki wao. unaweza kujumuika nao at ngoma4u@gmail.com, call +491788491992

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad