HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 5, 2023

MWANZA; MMOJA AJARIBU KUJIUA KWA KUJIKATA UUME

 

JESHI la Polisi Mkoa wa mwanza limesema kwamba mnamo Aprili Mosi  muda wa saa 20:00 Usiku huko kitongoji cha Kasuzu, kijiji na kata ya Namagondo, tarafa ya Mumulambo wilayani Ukerewe, mwanaume aitwaye Anselumu Sebuka, miaka 42, Mkulima na mkazi wa Namagondo, alikutwa ndani ya chumbachake akiwa amejaribu kujiua kwa kukata uume wake kwa kutumia kisu chenye ncha kali.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza. Wilbroad W. Mutafungwa- SACP imesema kuwa inadaiwa Ansele Sebuka alikuwa anatuhumiwa na ndugu zake kuiba mali mbalimbali za familia yake na za jamii inayomzunguka na kwenda kuziuza pamoja na ulevi uliokithili ambapo waliamua kumtenga kutokana na tabia zake mbaya. Baada ya tuhuma hizo ndipo aliamua kujikata uume wake kwa kisu na kuacha unaning’inia kwa lengo la kujiua. Chanzo cha tukio hilo ni ugonvi wa kifamilia uliopelekea mhanga kupata msongo wa mawazo.

Ansele Sebuka alipelekwa katika Hospitali ya wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kufuata njia sahihi za kutatua matatizo yao hususani kuwaona wataalamu wa afya ya akili ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msongo wa mawazo na kukosa uvumilivu wa migogoro mbalimbali katika jamii.

Katika tukio jingine taarifa hiyo imeeleza kuwa Tarehe Aprili 03, 2023 majira ya saa 12:00 mchana, kuliripotiwa tukio la mauaji ya Milembe Mihayo, miaka 11, mkazi Sumaha, baada kupigwa na baba yake mzazi siku ya tarehe 27.03.2023 majira ya saa 08:00 asubuhi katika kitongoji cha Ishungi kata ya Wala Wilayani Kwimba.

Baada ya kulipotiwa kwa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi lilifatilia kwa haraka na kufanikiwa kumkamata Mathayo Mishaka, miaka 40, Mkulima na mkazi wa kijiji cha Sumaha. Baada ya mahojiano ya kina na mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na mauaji ya binti yake kwa kumchapa na fimbo sehemu za mwili wake baada ya kumkuta nyumbani kwa babu yake mdogo aitwaye Dotto Masanyiwa akikokuwa ameagizwa, wakiwa bafuni na mvulana aliye kimbia baada ya kufumaniwa wakiwa wamevua nguo wakitaka kufanya mapenzi ndipo alipomkamata binti yake na kuanza kumpiga.

Milembe Mihayo aliendelea kupata maumivu makali bila kupelekwa Hospitali, ndipo baba yake huyo mzazi akamuagiza mke wake mdogo aitwaye Sofia Mashaka, Miaka 20, amkande miguu binti huyo iliyokuwa imevimba kutokana na kipigo na mama huyo alipomuuliza mmewe kuhusu tatizo hilo, alimueleza kuwa binti huyo huwa anasumbuliwa na tatizo la miguu kitendo ambacho mama huyu hakulizika nacho kwani alikuwa ameishi na binti huyo kwa muda wa mwaka mmoja bila kuona tatizo hilo.

Mwili wa Milembe Mihayo umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya kukamilishwa kwa upelelezi.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wazazi na walezi kuacha kutoa adhabu za kikatili kwa watoto wao badalayake watumie njia sahii ya kuwaonya pindi wanapokose ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza. Pia, linawaomba kuendelea kushirikiana kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad