HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 4, 2023

MRADI WA MAJI MWINDI WAZINDULIWA, KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA AWAPONGEZA RUWASA

Tenki lenye uwezo wa kuchukua lita 100,000 lililojengwa katika mradi wa maji Mwindi wilayani Mtwara ambalo litahudumia takribani wakazi 1,593 wa kijiji cha Mwindi.
Na Muhidin Amri, Mtwara
WAKAZI wa kijiji cha Mwindi na Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara,wameondokana na kero ya muda mrefu ya huduma ya maji safi na salama,baada ya wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Mwindi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim,meneja wa Ruwasa wilayani Mtwara Hamisi Mashindike alisema mradi huo utahudumia zaidi ya wananchi 3,465 kati yao 1,593 wanatoka kijiji cha Mwindi na 1,872 wa kijiji cha Mbawala.

Alisema,katika bajeti ya mwaka 2022 serikali kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uvico-19 imeipatia Ruwasa wilaya ya Mtwara jumla ya Sh.milioni 800,521,075 ili kutekeleza mradi huo.

Alisema,utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Januari na kukamilika mwezi Machi chini ya usimamizi wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) wilaya ya Mtwara.

Alieleza,mradi wa maji Mwindi ulianzishwa kwa lengo la kusogeza na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika umemaliza kabisa changamoto ya huduma hiyo kwa wakazi wa vijiji hivyo.

Kwa mujibu wake,mradi umehusisha ujenzi wa mateki mawili yenye ujazo wa lita 100,000 kila moja ambayo yamejengwa katika kijiji cha Mwindi ambapo moja ni la juu ya ardhi na lingine kwenye mnara wa mita 12.

Mashindike alitaja kazi nyingine zilizotekelezwa
ni ujenzi wa vituo(virula)12 vya kuchotea maji,ufungaji wa pampu mbili na kulaza mabomba ya maji umbali wa mita 14.363.

Alibainisha kuwa,kati ya fedha hizo Sh.milioni 302,077,979.00 zimetumika kununua pampu mbili na Sh.milioni 498,443,096.00 zimelipwa kwa mkandarasi ambapo wananchi wa vijiji hivyo wamechangia Sh.milioni 3.

Alisema,mradi umezingatia sera ya maji ya kumtua mama ndoo kichwani na umezingatia umbali usiozidi mita 400 kutoka kituo kimoja na kingine,na ameishukuru serikali kutoa fedha zilizofanikisha utekelezaji wa mradi huo.

Meneja wa Ruwasa alisema,mpaka sasa jumla ya kaya 21 na taasisi 7 zimeunganishiwa huduma ya maji majumbani ili kurahisisha uwepo wa maji karibu na kwenye makazi yao.

Aliongeza kuwa,kukamilika kwa mradi huo kutasaidia na kuwezesha wananchi hasa vijana na akina mama kuongeza ajira kwani watatumia maji hayo kulima bustani za mboga na hivyo kuinua kipato cha kaya husika na kuimarisha hali ya lishe katika jamii inayozunguka.

Pia alisema,mradi huo utawezesha kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kutoka asilimia 56.66 ya mwaka 2022 hadi asilimia 57.6 mwaka 2023,kutatua changamoto ya maji iliyokuwepo katika vijiji hivyo,kupunguza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko katika jamii kwa sababu ya kutumia maji safi na salama na kuchochea maendeleo ya watu na ustawi wake na kutoa ajira za muda mfupi 40 na muda mrefu 1.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim,amewapongeza wataalam wa Ruwasa kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango na weledi mkubwa kwani umeendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali.

Amewashukuru wananchi waliokubali kutoa ardhi yao bure ili kufanikisha mradi huo,na kuwataka wananchi wa mkoa wa Mtwara kuwa na utaratibu wa kujitolea nguvu zao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoibuliwa na kutekelezwa katika maeneo yao.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa,amewaasa wananchi wa vijiji hivyo kuhakikisha wanatunza mradi na kulinda miundombinu yake ambayo imetumia fedha nyingi za serikali ambazo zingeweza kupelekwa kwa wananchi wa maeneo mengine ambao bado wanakabiliwa na changamoto za huduma za kijamii.

Amewataka wataalam(Waandisi)wa maji kote nchini, kuwa na tabia ya kutembelea na kukagua mara kwa mara miradi inayojengwa ili kujiridhisha kama ina ubora unaotakiwa,badala ya kuwaachia mafundi na wakandarasi wanafanya kazi bila usimamizi wa karibu ili kuepuka miradi hiyo kujengwa chini ya kiwango.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Anafi Msabaha alisema,miaka ya nyuma serikali ilitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji,lakini baadhi ya miradi hiyo haikukamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubadhirifu.

Msahaba,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi ambazo zimesaidia kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa vijiji hivyo na wilaya ya Mtwara kwa ujumla.

Mkazi wa kijiji cha Mwindi Omari Mbonde,ameishukuru serikali kupitia Ruwasa mkoa wa Mtwara kuwajengea mradi huo ulimaliza kabisa kero ya huduma ya maji safi na salama iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Alisema baada ya kutekelezwa kwa mradi huo,sasa ndoa nyingi zitaimarika kwani hapo awali baadhi ya wanawake hawakupata muda wa kukaa pamoja na waume zao kwa kuwa walitumia muda mwingi kwenda kutafuta maji mtoni na kwenye visima vya asili.Picha no 616 Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mtwara Mhandisi Hamis Mashindike akionyesha mchoro wa mradi wa maji wa Mwindi unaohudumia zaidi ya wakazi 3,465 wa kijiji cha Mwindi na Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara,kulia mkimbiza Mwenge Kitaifa Juma Silima Sheha.

Picha no 619 Meneja wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilayani Mtwara Mhandisi Hamis Mashindike akieleza jambo kwa mkimbiza mwenge wa Uhuru Kitaifa Juma Silima Sheha,kabla ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim kufungua mradi wa maji Mwindi uliotekelezwa na Ruwasa kwa gharama ya Sh,milioni 800,521,075.

Picha no 623 Mkuu wa wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara Anafi Msabaha,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwindi(hawapo pichani)wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru kufungua mradi mkubwa wa maji kijijini hapo,kulia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Kaim.

Picha no 663 Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Kaim, akiondoa kitambaa kufungua rasmi mradi wa maji Mwindi kijiji cha Mwindi Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara,kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mtwara Erica Yegella.

Picha no 670 Meneja wa Ruwasa mkoa wa Mtwara Mhandisi Prim Damas wa sita mstari wa mbele,akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Ruwasa wilaya ya Mtwara na mkoa baada ya Mwenge wa Uhuru kufungua mradi wa maji Mwindi unaohudumia vijiji viwili vya Mwindi na Mbawala.

Picha no 593 Tenki lenye uwezo wa kuchukua lita 100,000 lililojengwa katika mradi wa maji Mwindi wilayani Mtwara ambalo litahudumia takribani wakazi 1,593 wa kijiji cha Mwindi.

Picha no 594 Moja kati ya vituo vya kuchotea maji kilichojengwa katika kijiji cha Mwindi wilayani Mtwara na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa).

Picha no 608 Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mwindi wilayani Mtwara,wafuatilia matukio ya uzinduzi wa mradi wa maji wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.

Na Muhidin Amri,
Mtwara

WAKAZI wa kijiji cha Mwindi na Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara,wameondokana na kero ya muda mrefu ya huduma ya maji safi na salama,baada ya wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kukamilisha ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Mwindi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim,meneja wa Ruwasa wilayani Mtwara Hamisi Mashindike alisema mradi huo utahudumia zaidi ya wananchi 3,465 kati yao 1,593 wanatoka kijiji cha Mwindi na 1,872 wa kijiji cha Mbawala.

Alisema,katika bajeti ya mwaka 2022 serikali kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya ugonjwa wa Uvico-19 imeipatia Ruwasa wilaya ya Mtwara jumla ya Sh.milioni 800,521,075 ili kutekeleza mradi huo.

Alisema,utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Januari na kukamilika mwezi Machi chini ya usimamizi wa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) wilaya ya Mtwara.

Alieleza,mradi wa maji Mwindi ulianzishwa kwa lengo la kusogeza na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama baada ya kukamilika umemaliza kabisa changamoto ya huduma hiyo kwa wakazi wa vijiji hivyo.

Kwa mujibu wake,mradi umehusisha ujenzi wa mateki mawili yenye ujazo wa lita 100,000 kila moja ambayo yamejengwa katika kijiji cha Mwindi ambapo moja ni la juu ya ardhi na lingine kwenye mnara wa mita 12.

Mashindike alitaja kazi nyingine zilizotekelezwa
ni ujenzi wa vituo(virula)12 vya kuchotea maji,ufungaji wa pampu mbili na kulaza mabomba ya maji umbali wa mita 14.363.

Alibainisha kuwa,kati ya fedha hizo Sh.milioni 302,077,979.00 zimetumika kununua pampu mbili na Sh.milioni 498,443,096.00 zimelipwa kwa mkandarasi ambapo wananchi wa vijiji hivyo wamechangia Sh.milioni 3.

Alisema,mradi umezingatia sera ya maji ya kumtua mama ndoo kichwani na umezingatia umbali usiozidi mita 400 kutoka kituo kimoja na kingine,na ameishukuru serikali kutoa fedha zilizofanikisha utekelezaji wa mradi huo.

Meneja wa Ruwasa alisema,mpaka sasa jumla ya kaya 21 na taasisi 7 zimeunganishiwa huduma ya maji majumbani ili kurahisisha uwepo wa maji karibu na kwenye makazi yao.

Aliongeza kuwa,kukamilika kwa mradi huo kutasaidia na kuwezesha wananchi hasa vijana na akina mama kuongeza ajira kwani watatumia maji hayo kulima bustani za mboga na hivyo kuinua kipato cha kaya husika na kuimarisha hali ya lishe katika jamii inayozunguka.

Pia alisema,mradi huo utawezesha kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kutoka asilimia 56.66 ya mwaka 2022 hadi asilimia 57.6 mwaka 2023,kutatua changamoto ya maji iliyokuwepo katika vijiji hivyo,kupunguza uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko katika jamii kwa sababu ya kutumia maji safi na salama na kuchochea maendeleo ya watu na ustawi wake na kutoa ajira za muda mfupi 40 na muda mrefu 1.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Kaim,amewapongeza wataalam wa Ruwasa kwa kutekeleza mradi huo kwa viwango na weledi mkubwa kwani umeendana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa na serikali.

Amewashukuru wananchi waliokubali kutoa ardhi yao bure ili kufanikisha mradi huo,na kuwataka wananchi wa mkoa wa Mtwara kuwa na utaratibu wa kujitolea nguvu zao na kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi ya maendeleo inayoibuliwa na kutekelezwa katika maeneo yao.

Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Kitaifa,amewaasa wananchi wa vijiji hivyo kuhakikisha wanatunza mradi na kulinda miundombinu yake ambayo imetumia fedha nyingi za serikali ambazo zingeweza kupelekwa kwa wananchi wa maeneo mengine ambao bado wanakabiliwa na changamoto za huduma za kijamii.

Amewataka wataalam(Waandisi)wa maji kote nchini, kuwa na tabia ya kutembelea na kukagua mara kwa mara miradi inayojengwa ili kujiridhisha kama ina ubora unaotakiwa,badala ya kuwaachia mafundi na wakandarasi wanafanya kazi bila usimamizi wa karibu ili kuepuka miradi hiyo kujengwa chini ya kiwango.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Anafi Msabaha alisema,miaka ya nyuma serikali ilitoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maji,lakini baadhi ya miradi hiyo haikukamilika kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ubadhirifu.

Msahaba,amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kutoa fedha nyingi ambazo zimesaidia kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa vijiji hivyo na wilaya ya Mtwara kwa ujumla.

Mkazi wa kijiji cha Mwindi Omari Mbonde,ameishukuru serikali kupitia Ruwasa mkoa wa Mtwara kuwajengea mradi huo ulimaliza kabisa kero ya huduma ya maji safi na salama iliyokuwepo kwa muda mrefu.

Alisema baada ya kutekelezwa kwa mradi huo,sasa ndoa nyingi zitaimarika kwani hapo awali baadhi ya wanawake hawakupata muda wa kukaa pamoja na waume zao kwa kuwa walitumia muda mwingi kwenda kutafuta maji mtoni na kwenye visima vya asili.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Mtwara Mhandisi Hamis Mashindike akionyesha mchoro wa mradi wa maji wa Mwindi unaohudumia zaidi ya wakazi 3,465 wa kijiji cha Mwindi na Mbawala Halmashauri ya wilaya Mtwara,kulia mkimbiza Mwenge Kitaifa Juma Silima Sheha.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara Anafi Msabaha,akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mwindi(hawapo pichani)wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru kufungua mradi mkubwa wa maji kijijini hapo,kulia Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Kaim.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdala Kaim, akiondoa kitambaa kufungua rasmi mradi wa maji Mwindi kijiji cha Mwindi Halmashauri ya wilaya Mtwara mkoani Mtwara,kulia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mtwara Erica Yegella.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad