HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 27, 2023

LOIBORSOIT WANAHITAJI SOKO-DIWANI KIDUYA

 


Na Mwandishi wetu, Simanjiro
DIWANI wa Kata ya Loiborsoit Wilayani Simanjiro Mkoani Manayara, Baraka Siria Ole Kiduya amesema wakazi wa eneo  hilo wana uhitaji mkubwa wa soko kwani wanafuata umbali mrefu huduma hiyo.

Kiduya ameyasema hayo wakati akisoma taarifa ya miezi mitatu iliyopita ya kata hiyo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Amesema wananchi wa kata hiyo wana uhitaji mkubwa wa soko kutokana na masoko yanayotoa huduma kwa jamii kuwa umbali mrefu na eneo hilo.

“Soko linalotoa huduma hivi sasa lipo mbali kwenye wilaya jirani ya Same mkoani Kilimanjaro liitwalo Kwasakwasa,  hivyo tunapaswa na sisi kuwa na soko letu,” amesema Diwani Kiduya.  

Pia, amesema wananchi wa kata hiyo wanauhitaji mkubwa wa kuwa na kituo cha afya ili waweze kupata matibabu pindi wakiugua na huduma nyingine kwani wana zahanati pekee.

Amesema kwenye idara ya elimu wana upungufu wa vyumba viwili vya madarasa kwenye shule ya msingi Ngage, vyumba vinne shule ya msingi Ndepes, vyumba viwili shule ya Loiborsoit B, na vyumba viwili shule ya msingi Mazinde.

“Kuna upungufu mkubwa wa matundu ya choo na mabweni mawili ya shule ya sekondari Loiborsoit na upungufu wa walimu kwenye shule zote za msingi za kata,” amesema Kiduya.

Amesema kwa kipindi cha miezi mitatu iliyopita hakukuwa na taarifa ya mwanafunzi yeyote wa shule ya msingi au sekondari kupata mimba shuleni.

Amesema uanzishwaji wa mradi wa shule mpya ya msingi Songoyo unatekelezwa kwa nguvu za wananchi na nyumba mbili ndani ya moja ya walimu Losokoni ipo hatua ya jamvi.  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad