HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 19, 2023

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UJENZI WA JENGO LA KLINIKI YA HUDUMA ZA MENO NA KINYWA NAMTUMBO

 

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdala Shaib Kaim kulia na Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Ngolo Malenya kushoto, wakiondoa kitambaa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la kliniki ya huduma ya meno na kinywa katika Hospitali ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Muonekano wa jengo la Kliniki ya huduma za meno na kinywa linalojengwa katika Hospitali ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma likiwa hatua ya mwisho kukamilika.

Na Muhidin Amri,, Namtumbo
SERIKALI imetoa kiasi cha Sh.milioni 320,643,000 kwa ajili ya kujenga jengo la kliniki ya afya ya kinywa na meno katika Hospitali ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma ikiwa ni mkakati wake wa kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa jengo hilo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdala Shaib Kaim,Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt Christopher Wabwarumy amesema,ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Mei mwaka jana na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 April mwaka 2023.

Amesema,madhumuni ya ujenzi wa mradi huo ni kuendelea kuboresha huduma za afya katika wilaya ya Namtumbo kwa kutoa huduma bora za afya kwa wakazi wa wilaya hiyo.

Dkt Wabwarumy,ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwa kuendelea kujenga Hospitali,vituo vya afya na Zahanti.

Aidha,amemshukuru Rais Dkt Samia kutoa fedha hizo ambazo zitatumika kutekeleza mradi huo mkubwa na muhimu unaotegemewa kuchochea kasi na ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa Namtumbo,mkoa wa Ruvuma na nchi kwa ujumla.

Kwa upande wake Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2023 Abdala Shaib Kaim,ameiagiza Halmashauri ya wilaya Nantumbo kusimamia ujenzi wa jengo hilo ili wananchi waanze kupata huduma za afya.

Alisema,serikali kuu kupitia wizara ya afya imetimiza wajibu wake kwa kutoa fedha za mradi huo,kwa hiyo kilichobaki kwa sasa ni viongozi wa wilaya ya Namtumbo kuhakikisha wanamsimamia fundi aliyepewa kazi ya kujenga mradi huo ili aweze kukamilisha haraka.

“ujenzi wa mradi huu uko nyuma sana takribani miezi miwili,nawaomba sana viongozi wa Namtumbo muwe karibu na fundi akamilishe kazi haraka ili wananchi waanze kupata huduma za afya”amesema.

Baadhi ya wakazi wa Namtumbo wamesema,jengo hilo litakapokamilika litawawezesha kupata huduma karibu badala ya kwenda wilaya nyingine za mkoa wa Ruvuma kufuata huduma za kinywa na meno.

Said Rajabu amesema,kukosekana kwa huduma hizo wilayani humo kuna waleta usumbufu na kero kubwa ambapo kwa sasa wanalzimika kwenda hadi Hospitali ya Rufaa ya mkoa(Homso)iliyopo umbali wa kilomita 67.

Abdala Kajala,ameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa mradi huo ili uweze kuwarahisishia upatikanaji wa huduma kwani wamechoka kutembea kwenda maeneo mengine kwa ajili ya kufuata huduma za maeneo na kinywa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad