
Picha za pamoja za Wafanyakazi wa DART katika wakati wa zoezi la Usafi katika Kituo Mlishi cha Shekilango Jijini Dar es Salaam. *Dkt. Mhede ataka wananchi kuendelea kuheshimu miundombinu na miti katika barabara
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) umesema kuwa walioharibu miundombinu ya mradi ya mabasi yaendayo haraka (BRT) kwa kuegesha magari wairejeshe ili kujiondolea usumbufu utawaokuta.
Hayo ameyasema Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Dkt.Edwin Mhede wakati maadhimisho ya Muungano ambapo kwa DART ilikuwa kukagua Miti iliyopandwa kutoka Kituo cha Basi Usalama hadi Makao Makuu ya Wakala yaliyopo Ubungo Maji jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa miundombinu wametoa kwa wale waliofanya sehemu ya kando kando ya mradi wa barabara ya Morogoro kuwa ni maegesho ambapo sheria iko wazi hivyo warejeshe mara moja kabla ya sheria haijachukua mkondo wake.
Dkt.Mhede ambaye ametembea kukagua miti pamoja na wafanyakazi wa DART kutoka Magomeni Usalama hadi Ubungo Maji ikiwa ni pamoja na kushirikisha wananchi kupata maoni yao katika utunzaji wa miti na barabara ya mabasi yaendayo haraka.
Amesema serikali imetumia fedha katika upandaji wa miti lakini baadhi ya wananchi waliokuwa nyuma wameharibu hali ambayo inaonyesha hakuna usimamizi na kufanya Dar es Salaam isiwe ya kijani.
Aidha amesema kuwa kuwa miti iliyokauka au kuharibiwa watairejesha lakini kwa kuhakikisha wale ambao wako nyuma wanafanya biashara nyuma kuwa sehemu ya wasimamizi wa ustawishaji wa miti itakayopandwa katika
awamu nyingine.
Dkt.Mhede amesema kuwa wananchi na vikundi mbalimbali wanaendelea kushirikiana katika utunzaji wa miundombinu na upandaji wa miti.
Mmoja wa Mwananchi Jackson Joseph amesema kuwa wanashukuru DART kwa kupanda miti ambayo baadae itatumika kwa kivuli na kuifanya Dar es Salaam ya Kijani kutokana na kampeni ya upandaji miti nchi nzima.
Amesma kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakiharibu miundombinu ya serikali ikiwemo na miti bila kutambua wanachofanya ni ukwamishaji wa maendeleo.


Wafanyakazi wa DART wakifanya usafi katika Kituo Mlishi cha Shekilango jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Dkt.Edwin Mhede akizungumza na wananchi katika eneo la Mwembechai katika Sikukuu ya Maadhimisho ya Muungano kati Tanganyika na Zanzibar kuhusiana na utunzaji wa miti iliyopandwa katika barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment