HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, April 2, 2023

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM NDAKI YA SAYANSI ZA JAMII KUZINDUA KITABU APRILI 4, 2023

 Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam kuelekea uzinduzi wa Kitabu kitakacho zinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo. Katikati ni Mhadhiri kutoka Indara ya Geografia, Faraja Namkesa na Mhadhiri wa Idara ya Sosiolojia na Antrolojia, Ndaki ya Sayansi za Jamii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Rechard Sambaiga.


CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Ndaki ya Sayansi za jamii kuhitimisha mradi wa ’Ushirikiano Mpya katika Uhifadhi na Maendeleo ya Kiikolojia na Jamii’ yaani New Conservation Partnerships for Sustainability (NEPSUS) kwa kuzindua kitabu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2023 jijini Dar es Salaam, Rasi wa Ndaki ya Sayansi za Jamii, Profesa Christine Noe amesema kuwa Kitabu hicho kitazinduliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa (MB) Aprili 4, 2023 chuoni hapo.

Amesema kuwa Uzinduzi wa kitabu hicho utakuwa unahitimisha miaka mitano ya mradi wa utafiti ulioanza 2016 hadi 2020 uliojikita katika katika sekta tatu za maliasili ambazo ni misitu, wanyamapori na mazao ya baharini.

Prof. Noe amesema kuwa Washirika katika mradi huo walikuwa watafiti ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Idara za Jiografia, Sayansi ya Siasa na ile ya Kilimo na Uvuvi) wakishirikiana na watafiti kutoka Shule Kuu ya Biashara ya Copenhagen, Chuo Kikuu cha Sheffield huko Uingereza, Chuo Kikuu cha Roskilde, Denmark na Chuo Kikuu cha Lafayette, Marekani.

Amesema miongo mitatu kumekuwa na ongezeko kubwa la ushirikishwaji wa jamii katika kuhifadhi wa maliasili na pia washirika kutoka taasisi mbalimbali duniani wameungana na serikali ya Tanzania katika kubadili mtazamo na mwenendo wa uhifadhi.

Akizungumzia malengo ya mradi huo uliofanyika katika wilaya tatu ambazo ni Rufiji, Kilwa na Mtwara Vijijini amesema kuwa ilikuwa lilikuwa kuangalia kama ongezeko la ushirikiano katika shughuli za kuhifadhi wa maliasili umeongeza ufanisi au la katika kuimarisha uhifadhi wenyewe na maendeleo ya jamii.

Prof. Christine amesema kuwa Kukumekuwa na matarajio makubwa na rasilimali nyingi zimetumika kuwekeza kwenye juhudi hizi za kuimarisha ushirikiano katika shughuli za uhifadhi.

Hata hivyo, haipo wazi kama juhudi hizo za wadau mbalimbali na mifumo iliyotengenezwa kuwezesha utekelezaji wa ushirikiano wa wadau katika kuhifadhi zimezaa matunda mazuri na endelevu hususan kwa maliasili zenyewe na maendeleo ya jamii.

“Kitabu hiki kinaonyesha ni namna gani juhudi za ushirikiano wa wadau wa hifadhi zimekuwa na matokeo tofauti tofauti. Watafiti wa mradi wa NEPSUS nao ni wanataaluma katika nyanja tofauti na ushiriki wao katika mradi kumewezesha uchakataji wa taarifa kwa namna tofauti. Kitabu hiki kimechakata taarifa za kila sekta kuangalia kama ushirikishwaji wa jamii na ongezeka la wadau mbalimbali kwenye uhifadhi wa maliasili kumeleta matokeo chanya kwa kimazingira na maisha ya watu. Je,sehemu zenye ushirikiano wa wadau wengi knatofauti gani na sehemu zenye ushirikiano wa wadau wachache? Na vipi kuhusu sehemu zisizo na ushirikiano kabisa katika kuhifadhi ilihali kuna maliasili?”

Katika kutafiti ushirikiano wa wadau, mifano iliyotumika kuelezea namna wadau wanavyoshirikiana ni Jumuiya za Jamii za wanyamapori (yaani Wildlife Management Areas (WMAs) wilayani Rufiji): Jumuiya za Usimamizi Shirikishi wa Msitu kwa Jamii (yaani Community-Based Forest Management (CBFM) wilayani Kilwa) na Vikundi vya Usimamizi Shirikishi wa Bahari (yaani Beach Management Units (BMUs) Mtwara Vijijini). Mifano hii iliwezesha kulinganisha ukuwaji wa ushirikiano na matokeo yake kwa kuzingatia historia za uhifadhi katika sekta, jiografia ya maenoe na tofauti za rasilimali husika, ambavyo vyote hivi vinahusika kwenye kufanikisha ama kukwamisha ushirikiano na matokeo ya kisera na kijamii. Ulinganifu katika sekta hizi tatu pia uliwezesha kupata uelewa mpana wa usimamizi wa maliasili za taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad