WHMTH-Dar es Salaam
Waziri
wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye (Mb)
amesema Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na
wawekezaji katika sekta ya mawasiliano ambao wanaleta mageuzi.
Waziri
Nape amesema hayo jijini Dar es Salaam alipotembelea kituo cha mkongo
wa mawasiliano cha 2 Afrika kinachosimamiwa na Kampuni ya Airtel ambapo
kukamilika kwake kutawezesha kuunganisha nchi zaidi ya 30 Afrika.
"Kwanza
niwapongeze Airtel kwa kuliona hili ambalo litaleta mageuzi makubwa
kwenye sekta ya Mawasiliano, mkongo huu utakuwa wenye kasi zaidi na
utasaidia kuunganisha watu kwa mataifa tofauti, hivyo naamini utatatua
kwa kiwango kikubwa changamoto za kimawasiliano"- amesema Waziri Nape.
Waziri
Nape ameongeza kuwa kuongezeka kwa mkongo uliopita chini ya Bahari ni
dalili nzuri kwani watoa huduma kama vile mitandao ya simu watakuwa na
nafasi ya kufanya machaguo juu ya mkongo upi utumike kitu ambacho
kinaweza kuchangia kushuka kwa gharama na kuongezeka kwa ubora wa huduma
za Intaneti.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Dinesh Balsingh amesema mkongo
huo utakuwa mkombozi na utaleta mageuzi makubwa katika sekta ya
mawasiliano.
"Tunaendelea
kushirikiana na serikali katika kuhakikisha mwananchi anapata unafuu
katika mawasiliano, hivyo kampuni zote za mawasiliano zinaweza kutumia
mkongo huu ili tuzidi kumpunguzia gharama mwananchi"-amesema Dinesh.Matukio
mbalimbali katika picha wakati Waziri wa Habari, Mawasiliano na
Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akikagua kituo cha
Uendeshaji Mkongo wa Mawasiliano cha cha 2 Afrika kinachomilikiwa na
Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo 24
Machi, 2023.
Waziri
wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
akikagua sehemu unapoingilia Mkongo wa Mawasiliano wa Baharini iliyopo
Mbezi Beach kuelekea kituo cha uendeshaji cha 2 Afrika kinachomilikiwa
na Kampuni ya Airtel Tanzania kilichopo Mbezi jijini Dar es Salaam leo
24 Machi, 2023.
No comments:
Post a Comment