HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 20, 2023

TASAC, WIZARA YA UJENZI NA UCHUKUZI WAWANOA WAKUFUNZI DMI

TASAC kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wawanoa wakufunzi 23 kutoka Chuo Cha Baharia cha Dar es Salaam (DMI) kwa siku nne mfurulizo.

Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20,2023 wakati wa kufungua mafunzo kwa wakufunzi hao amesema kuwa mafunzo hayo yatasaidia wahitimu kuwa mahiri katika tasnia ya bahari na kupelekea kupata kazi katika nchi mbalimbali.

"Mabaharia wataokuwa wanatoka katika chuo chetu wanaweza kupata soko la ajira za kufanya kazi kwa sababu watakuwa wamepata elimu kutoka kwa walimu ambao wamepata mafunzo kutoka kwa wataalamu kutoka nchi mbalimbali." Amesema Mkeyenge.

Amesema katika Mafunzo hayo wapo Wafanyakazi wa TASAC ambao watahusika katika kutoa vyeti, wajumbe wa bodi ya usahishaji mitihani ya mabaharia na wawakilishi kutoka Wizara ya uchukuzi, sekta ya uchukuzi.

Akizungumzia Manufaa ya Mafunzo yanayotolewa na shirika la Bahari dunia, Mkeyenge amesema kuwa mafunzo hayo yanasaidia kuitangaza nchi.

Amesema kuwa awali kulikuwa hakuna ukaribu na wajumbe mbalimbali kutoka shirika hilo duniani na kwa sasa ukaribu uliopo utachangia mabadiliko makubwa katika sekta ya bahari na utalii.

Amesema mafunzo mengine ya uongozi na utafutaji wa ajali zinapotokea kwenye maji yatafanyika Aprili mwisho mwaka huu kwa wafanyakazi waliopo katika sekta ya bahari.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Habari Dar es Salaam, Dkt. Tumaini Gurumo ametoa wito kwa vijana wa kitanzania, Wazazi, walezi waone fursa iliyopo katika upande wa mabaharia ili kuondoa vijana mtaani na kupata ajira kimataifa.

Amesema cheti anachokipata Baharia wa kitanzania anakuwa amepanua wigo wa kupata ajira ndani na nje ya nchi.

"Baharia aliyesoma katika Chuo cha DMI anatambulika katika meli yeyote ulimwnguni, kwahiyo kunawigo mpana wa ajira na nafasi za mabaharia bado zipo nyingi." Amesema Dkt. Tumaini

Akizungumzia mafunzo amesema kuwa Mafunzo yanayotolewa leo ni utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa 1978 unatoa miongozo ya namna elimu na mafunzo ya mabaharia yaendeshwe.

"Na sisi Tanzania tumeriadhia mkataba huo na sasa tuanautekeleza."

Amesema kuwa wanakazi kubwa ya kuendelea kutekeleza mkataba na kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa.

Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akifungua mafunzo kwa wanaofundisha Chuo cha Habari Dar es Salaam(DMI) jijini Dar es Salaam leo Machi 20,2023.
Mahadhiri wa Chuo cha Habari Dar es Salaam(DMI) Mhandisi Juma Kapaya akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2023.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Habari Dar es Salaam, Dkt. Tumaini Gurumo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20,2023 wakati wa kufungua mafunzo kwa wakufunzi.
Mkurugenzi wa Mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 20,2023 wakati wa kufungua mafunzo kwa wakufunzi.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad