HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 28, 2023

Rais Samia Atunukiwa Tuzo Maalum



Na Ahmed Sagaff – MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum kutokana na juhudi zake za kuimarisha uhuru wa habari na haki ya wananchi kupata taarifa za kweli na sahihi.

Tuzo hiyo imetolewa na Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini katika hafla ya ufunguzi wa Kikao Kazi cha Maafisa hao kilichoanza leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amekabidhi tuzo hiyo kwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amepokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia.

Akiizungumzia tuzo hiyo, Waziri Nape ameeleza, “Tunatambua kazi nzuri inayofanywa na Rais, tunatoa tuzo hii tukitambua mchango wake katika kuimarisha uwazi kwa mambo yanayofanywa na Serikali, tumeshuhudia fedha zinakopwa na kutangazwa hadharani zinakwenda kufanya nini, huu ni uwazi mkubwa kabisa.”

“Tunatoa tuzo hii ili kutambua mchango wake katika kuhakikisha Watanzania wanakuwa na wigo mpana wa kupata taarifa za kweli na sahihi,” ameongeza Waziri Nape.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea tuzo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kwa kutambua mchango wake katika nyanja mbalimbali ikiwemo tasnia ya habari, Uhusiano wa Kimataifa, Siasa, ukuaji wa uchumi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, wakati wa kikao kazi cha maafisa hao. Kushoto ni Spika Dkt. Tulia Ackson na Kulia ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kwenye kituo cha Kimataifa cha Julius Nyerere Dar es Salaam, Machi 27, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad