HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 28, 2023

PAC YARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI MRADI WA TEMEKE KOTA


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa maelezo ya utekelezaji wa mradi huo kwa kamati hiyo na kueleza kuwa wamepokea maelekezo yaliyotolewa katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati. Leo jijini Dar es Salaam.

 *Yaeleza mradi huo utapunguza uhaba wa nyumba za makazi


KAMATI Ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC,) imeeleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya watumishi wa Umma, 'Temeke Kota' mradi unatekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA.)

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi na kukagua mradi huo Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhandisi. Isack Kamwelwe (mb) amesema, mradi huo unatekelezwa kwa fedha za Umma zilizopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


"Kamati imeridhishwa na hatua iliyofikiwa, mradi huu wa miezi 24 hadi leo umekamilika kwa asilimia 19... Jengo moja la sakafu 9 litachukuwa kaya 144 na majengo saba yatajengwa hapa tunategemea mradi huu utapunguza uhaba wa nyumba za makazi kwa watumishi wa Umma na watanzania kwa ujumla kama ilivyokuwa kwa mradi wa Magomeni Kota." Amesema.


Ameeleza, ndani ya miezi 24 jengo moja litakamilika kwa gharama za shilingi Bilioni 5 na tayari TBA imepokea Bilioni 4.3 za utekelezaji wa mradi huo.


" Baada ya kupokea taarifa na kutembelea mradi huu kamati imeridhishwa na kinachoendelea, msingi umekamilika pamoja na tanki la kuhifadhi maji kwa makazi haya umekamilika, Hizi ni fedha za Umma hivyo watumishi na watanzania ni wanufaika wa jitihada hizi za Serikali chini ya TBA." Amesema.


Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA,) Arch. Daud Kondoro amesema, Wakala imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo uliokamilika kwa asilimia 19 na kupokea maelekezo yaliyotolewa na kamati hiyo ikiwemo mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa mradi kwa wakati.


Mradi wa Temeke Mwisho unatekelezwa kwa fedha za Serikali na utagharimu Bilioni shilingi 19.4 ambapo hadi sasa Wakala hiyo imepokea Bilioni 4.3 na utakapokamilika utabeba Kaya 144 na inategemewa kujengewa majengo 7 zaidi yatakayobeba Kaya 1000.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC,) Mhandisi. Isack Kamwelwe (mb,) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua mradi huo uliokamilika kwa asilimia 19 na kueleza kuwa Serikali itatoa fedha zitakazokamilisha utekelezaji wa mradi huo kwa manufaa ya watanzania, Leo jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC,) wakipata maelekezo ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa wataalam wa TBA.
Ujenzi wa mradi huo ukiendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad