HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 30, 2023

NBAA YAPOKEA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKISHO LA WAHASIBU LA AFRIKA

 


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imepokea wajumbe wa Bodi ya  Shirikisho la Afrika ‘Pan African Federation of Accountants (PAFA)’ waliokuja nchi kwa lengo la kufanya kikao cha Bodi ya Wakurugenzi kuzungumzia mambo mbalimbali ya Taaluma ya Uhasibu katika bara la Afrika. 

Akizungumza Mkurugenzi Mtendaji  wa NBAA, CPA Pius Maneno amesema, wajumbe hao na wasaidizi wao wa jopo la watu wapatao ishirini na tatu, wapo nchini kwa kikao cha siku tatu kujadili mambo mbalimbali yahusiyo Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi.

Uongozi wa juu wa Shirikisho hilo pia unaoongozwa na Rais Bw. Cosme Goundete kutoka Benin, Bi. Keto Kayemba Makamu wa Rais toka Uganda na Bi. Alleta Maria Prisloo kutoka Afrika ya Kusini, ulikutana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Tanzania akiwemo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mkaguzi wa Ndani wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya dhamana ya masoko ya mitaji na kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo ya Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi.

Sambamba na hilo, wajumbe hao wameshuhudia uzinduzi wa miundo mbinu ya kufundishia kwa njia ya mtandao iliyojengwa na NBAA katika jengo la Mhasibu Dar es Salaam ambapo mafunzo na semina mbalimbali zitakuwa zikiendeshwa mtandaoni na kufikiwa na wadau wote duniani kote ikiwa na lengo la kuendana na na mabadiliko ya kiteknolojia ya kuhamishia shughuli na huduma zake kidigitali ili kufikika kirahisi

Aidha, Afisa Masoko na Mawasiliano, Bi. Magreth Kageya, ameongezea kuwa Shirikisho hilo la Afrika kutembelea Tanzania chini ya mwenyeji wake NBAA, imekuwa ni fursa kubwa kwa Tanzania kujitangaza na pia ni jambo kubwa kwa Taaluma ya Uhasibu kwani ziara hiyo itasaidia kwenye mipango mbalimbali ya kuendelea Taifa na Taaluma ya Uhasibu na Ukaguzi kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius Maneno akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya  Shirikisho la Afrika ‘Pan African Federation of Accountants (PAFA) wakiongozwa na Rais  wa Shirikisho hilo Bw. Cosme Goundete kutoka Benin, Bi. Keto Kayemba Makamu wa Rais toka Uganda na Bi. Alleta Maria Prisloo kutoka Afrika ya Kusini
Matukio mbalimbali ya mkutano wa wajumbe wa Bodi ya  Shirikisho la Afrika ‘Pan African Federation of Accountants (PAFA) uliofanyka katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) ikiwa kama mwenyeji wa mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius Maneno akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Afrika ‘Pan African Federation of Accountants (PAFA) Bw. Cosme Goundete kutoka Benin mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Bodi hiyo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad