HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 8, 2023

NBAA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2023

  

Katika kuadhimisha siku hiyo Wanaw
ake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wameshiriki maadhimisho hayo yaliyofanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es Salaam. . Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ubunifu na mabadiliko ya teknolojia: chachu ya kuleta usawa wa kijinsia. Kupitia kauli mbiu hii inatukumbusha kuona umuhimu wa ujumuishi wa wanawake katika masuala ya teknolojia. Kwa upande mwingine
, inatukumbusha kufanya tafakuru juu ya namna teknolojia ni kichocheo au kizuizi cha kujileta usawa wa kijinsia.

Tarehe 8 Machi ya kila mwaka ni Siku ya wanawake duniani, ambapo siku hii inataka kukumbushia na kutafakari juu ya matokeo ya kisiasa, kijamii, kiuchumi waliyofikia wanawake na msimamo wao imara katika ngazi ya kijamii kwa ujumla.

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mwenyekiti wa Wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA, Irene Mutagaywa amewataka wanafunzi walioko mashuleni kujikita katika kutengeneza ndoto zao kwa kusoma kwa bidii hasa masomo ya Sayansi ili kuweza kuendana na teknolojia inayoendelea kukua siku baada ya siku

Siku ya wanawake duniani ilianza kutokana na jitihada za wanawake 15,000 mwaka 1908 walipoandamana mjini New York Marekani wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, ujira wa kuridhisha na haki ya kupiga kura. Kilikuwa ni chama cha kisoshalisti cha Amerika kilichotangaza kuwa ni siku ya kwanza ya kitaifa ya wanawake, mwaka mmoja baadaye. Wazo la kuwa siku ya kimataifa lilianzishwa na mwanamke kwa jina la Clara Zetkin. Yeye alipendekeza wazo hilo mwaka 1910 katika mkutano wa kimataifa wa wafanyakazi wanawake huko Copenhagen Denmark.

Picha mbalimbali  za matukio ya wafanyazi wanawake wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika leo Machi 08, 2023 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad