HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 13, 2023

KAMANDA WA POLISI MBEYA AFUNGA MASHINDANO POLISI JAMII SUPER CUP, 2023

 

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga, Machi 12, 2023 wilayani Rungwe amefunga mashindano ya mpira wa miguu yaliyojulikana kwa jina la Polisi Jamii Super Cup 2023.

Akifunga mashindano hayo yaliyoshirikisha timu nane kutoka vijiji viwili vya Ntokela na Nzunda vilivyopo Kata ya Ndanto, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Kamanda Kuzaga amewataka vijana kupenda kushiriki michezo kwani ni ajira, uimarisha afya na ujenga ushirikiano na mshikamano miongoni mwa wananchi.

Aidha kamanda Kuzaga ametumia hadhira iliyofika kushuhudia fainali hiyo kuwataka wananchi wa kata ya Ndanto kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuzuia na kutanzua uhalifu kwa kumpa ushirikiano mkaguzi wa kata aliyepo.

Kwa upande wa Afisa ushirikishwaji jamii Mkoa wa Mbeya ACP George Salala amempongeza Mkaguzi Kata ya Ndanto A/Insp.Ezekiel Lomnyack pamoja na uongozi wa kata kwa namna walivyoshirikiana kuratibu na kufanikisha kufanyika mashindano hayo yenye lengo la kuwakutanisha vijana pamoja, kuwapa elimu ya Polisi Jamii ambayo itasaidia kuwaepusha na uhalifu.

Mashindano ya "Polisi Jamii Super Cup, 2023" yalianza rasmi Februari 15, 2023 na kushirikisha timu nane ambapo fainali imekutanisha timu ya Swebo dhidi ya Mji mwema ambapo Swebo fc wameibuka mabingwa kwa ushindi wa magoli 3 dhidi ya 2. Awali mapema Januari 2023 mashindano kama hayo yalifanyika Kata ya Ilemi Jijini Mbeya na kuhusisha timu za mitaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad