HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 10, 2023

Diwani Chimba ampigia magoti Chongolo kushinikiza mambo Makuu Matatu

 Na Mary John, Mirerani

DIWANI wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Lucas Zacharia Chimba amelazimika kumpigia magoti Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo kushinikiza mambo makubwa matatu moja likiwa ni kupandisha hadhi Kituo Cha Afya Cha Endiamtu kuwa Hospitali teule,ambapo kwa sasa kinahudumia wagongwa 260 - 300 Kwa siku.

Akizungumza Jana mbele ya Katibu Mkuu, Diwani Chimba alisema wakati umefika wa Serikali kukiangalkia Kwa jicho la huruma Kituo Cha Afya Cha Endiamtu kwani kinahudumia Wilaya 3 Kata 8.

Chimba alisema Kituo hicho Kwa sasa kimezidiwa kinahudumia wagonjwa wagonjwa 260 hadi 300 Kwa siku, hali inavyoelekea hata baadhi ya huduma kuzolota .

" Mh.Katibu wetu hata ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliahidi kuwa Kituo Cha Afya Cha Endiamtu kupandishwa hadhi kuwa Hospitali teule, tunaomba kiongozi wetu uliangalie hili Kwa jicho la pekee na la huruma wananchi wanateseka sana.

Aidha alisema Kituo hiko kinahudumia Kata nane ikiwa ni pamoja na Kata ya Shambarai, Mbuguni (Wilaya ya Arumeru), Makiba ( Wilaya ya Arumeru ), Majengo (Wilaya ya Arumeru), Mtakuja ( Hai ) ,Naisinyai, Mirerani na Endiamtu yenyewe.

Aidha alisema Kituo hiko Cha Afya hakina Wodi akina mama wote na wagonjwa wengine wanateseka wanategemea kwenda Wilaya ya Hospitali ya Hai, Kilimanjaro,na Mount Meru, hivyo ameomba hilo suala likamilike isiwe ahadi tena.

Akizungumzia suala la pili Maji Diwani Chimba alisema kunantatizo la maji, watu ni wengi maji hakuna, kwenye shule hakuna maji, ambapo alisema maji ndio kila kitu kwenye jamii, hivyo alimuomba Katibu Mkuu kuhakikisha analichukua hilo nankulifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili wananchi wawezenkuondokana na adha hiyo ya maji.

"Mh.Katibu Mkuu tunaomba utusaidie ili tupate maji, hatuji tatizo liko wapi, maji ndio kila kitu Mh.Katibu maji yakiwepo hayo Mengine yatawezekana, lakini tunachokuomba sasa hivi niko chini ya miguu yako nakupigia magoti Mh.Katibu, watu ni wengi sana maji hakuna.

Aidha alisema jambo la tatu ni Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani kuwa Halmashauri kamili, sifa ama vigezo vyote vimekamilika, wananchi wanafuata huduma za Kimahakama na nyingine kubwa na muhimu Orkesumet ambapo hadi kuifikia ni umbali wa km.122 kutoka Mirerani hadi Orkesumet ambapo ndio Makao Makuu ya Wilaya ya Simanjiro.

Alisema Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani Toka ilivyoanzishwa Mwaka 2008 hadi sasa 2023 wananchi wanapata changamoto yingi wanazokabiliana nazo za kufuata huduma ni mateso makubwa kwa jamii, hivyo Serikali iangalie uwezekano wa kuifanya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mirerani kuwa Halmashauri kamili ili kusogeza huduma muhimu na kubwa jirani na wananchi.

Akitoa ufafanuzi Chongolo alisema mambo ya bajeti huwa ni magumu hasa yanapokuja kuongeza masuala ya utawala.

" Si mnaona tofauti linalowezekana nasema hili linawezekana, lisilowezekana hili nasema labda Bilionea saniniu Laizer aniambie kuwa nitakupa bil.100 nitawaleteeni Halmashauri hata kesho, Sasa Laizer mwenyewe yuko tayari kutoa hiyo bil.100, mambo ya bajeti ni magumu hasa yanapokuja kuongeza masuala ya utawala, mnajua tunatakiwa tupeleke huduma bil.15 tafsili yake lazima ionekane kwenye huduma zaidi ili kipindi hiki yale tuliyoahidi yatokee" alisema Chongolo
Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo akisakimiana na Diwani wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara Lucas Zacharia Chimba ( ndiye aliyempigia magoti ) Katibu Mkuu kushinikiza mambo Makuu matatu ikiwemo la Kituo Cha Afya kipandishwe hadhi iwe Hospitali teule, suala la maji pamoja na Mamlakamya Mji Mdogo wa Mirerani kuwa Halmashauri kamili, Katibu Mkuu alikwenda kukagua Jengo la Tanzanite City katika Kata hiyo ya Endiamtu, Picha na Mary John


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad