HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 5, 2023

CCM YASEMA HADI JUNI ,2023 VITUO VYOTE VYA AFYA VITAKUWA VIMEPATA VIFAA TIBA

 


Na Mwandishi Wetu,Hanang

CHAMA Chama Mapinduzi (CCM)kimesema kwamba vituo vyoye vya ambavyo vimejengwa nchi nzima vitapelekewa dawa na vifaa tiba kwa lengo la kuhakikisha vinatoa huduma za matibabu ya afya kama ambavyo imekusudiwa.

Akizungumza leo Machi 5,2023 baada ya kutembelea Kituo cha afya Basotu kilichopo wilayani Hanang mkoani Manyara  Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo amesema hadi ufikia Juni 2023, vituo vya afya vilivyojengwa nchi vitapelekewa vifaa tiba.

Chongolo amesema tayari amewasiliana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akamweleza mpango wa serikali na Bohari Kuu ya Dawa (MSD) wa kuagiza kwa jumla vifaa tiba vitakavyosambazwa nchi nzima kwenye vituo vya afya,lengo kuhakikisha wananchi wanapata huduma.

Amesisitiza watahakikisha vituo vyote vya afya vinapata vifaa tiba kwani hawawezi kuwa na majengo mazuri lakini hayana huduma,hivyo Chama hicho kinachotaka kuona ni huduma bora zinatolewa ambazo zitaendana na uzuri wa majengo hayo.

"Serikali imejikita kwenye ujenzi wa vituo vya afya ili kutoa huduma ya afya ya uzazi salama kwa mama na mtoto sambamba na kupunguza vifo vyao hadi kufikia asilimia 0.Hivyo moja wajibu Wetu kama Chama ni kusimamia malengo hayo."

Chongolo wakati anaanza kuzungumza ameipongeza pia Halmashauri ya Hanang kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho kwa kutumia makusanyo ya ndani,majengo mazuri,yanavutia.

"Wamefanya hivi kwanini kwasababu Serikali Kuu imefanya kazi kubwa zifuatazo ndani ya Halmashauri ya Hanang ikiwemo kubeba jukumu la mishahara yote ya watumishi fedha zinatoka Serikali Kuu.

"Pia Serikali imeweka mpango kwa halmashauri ambazo uwezo uko chini asilimia 40 ya makusanyo ya ndani yanatakiwa kwenda kwenye miradi na halmashauri ambazo ziko juu asilimia 60 ya makusanyo inakwenda kwenye maendeleo."

Awali,Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Dk Mohamed Nkodi ameeleza kwamba zahanati ya Basutu ilijengwa mwaka 1999 na ilipofika mwaka 2006 ilipandishwa hadhi na kuwa kituo cha afya.

"Kituo hiki hakikutengewa fedha kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya majengo hadi kilipotengewa Sh.milioni 400 katika bajeti ya mwaka 2021/22.Ujenzi wa kituo hiki kimekamilika kwa asilimia 99, kilichobaki ni kupata vifaa tiba kwa ajili ya chumba cha upasuaji."

Katibu Mkuu wa ChamaCha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiangalia daftari maalum la wakina mama waliofika na kujifungua katika kituo cha afya Basotu wengine pichani ni Mganga Mkuu wa Wilaya yan Hanang (kulia) na katikati ni Muuguzi wa wodi ya wazazi Ndugu Nicodemus Ingi .

Katibu Mkuu wa ChamaCha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wanachama wa CCM na wakazi wa Hanang mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Afya  Basotu, Hanang mkoani Mara.
 
Sehemu ya wanachama wa CCM na wakazi wa Basotu waliojitokeza kumsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo ambaye pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa walifika Basotu na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Basotu.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad