HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 23, 2023

BENKI YA NMB 'YAMWAGA' MSAADA WA VIFAA MBALIMBALI ELIMU NA AFYA VYENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 39 KWA WILAYA ZA KANDA YA KATI

Benki ya NMB imetoa msaada vifaa mbalimbali kwa sekta za elimu na afya vyenye thamani ya shilingi milioni 39 kwa Wilaya za Kanda ya Kati zikiwemo Mpwapwa, Kondoa na Chemba ikiwa ni utekelezaji wa sehemu ya dhamira yake ya kurudisha kwa jamii.

Walionufaika katika Wilaya ya Mpwapwa ni pamoja na Shule za Msingi Iyoma na Mpwapwa zilizopokea madawati 100 kwa jumla yenye thamani ya shilingi milioni 10.

Walionufaika katika Wilaya ya Kondoa kwa upande mwingine ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ambayo iliyopokea mashuka 200 yenye thamani ya shilingi milioni 6, Shule za Sekondari Bicha, Masange, Kimaha na Dalai zilizopokea meza na viti 50 kila moja vyenye thamani ya shilingi milioni 5 huku Shule ya Msingi Lembo ikipata vifaa vya kuezekea vyenye thamani ya shilingi milioni 5.6.

Kwa upande wa sekta ya afya, benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 12.3 katika Hospitali ya Wilaya ya Chemba ambavyo ni pamoja na mashuka 64, vitanda vya kujifungulia vinne, vitanda vya kawaida vya wagonjwa 10, na magodoro 10 miongoni mwa vifaa hivyo kwa lengo la kuasaidia kuimarisha utoaji huduma hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NMB, Nsolo Mlozi alisema msaada huo unathibitisha dhamira ya benki hiyo ya kurudisha kwa jamii inapofanyia kazi na kuongeza kuwa benki hiyo imetenga shilingi bilioni 6.2 kusaidia uwekezaji katika uwekezaji katika miradi mbalimbali ya ya kijamii hususani katika sekta zake za kipaumbele ikijumuisha elimu, afya na dharura mwaka huu.

Wakati wa hafla hiyo Mlozi aliwataka wanufaika wa michango ya benki hiyo kuvitumia vyema vitu vilivyotolewa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Kizigo wakati akipokea msaada huo kwa niaba ya wilaya yake aliipongeza benki hiyo kwa ukarimu wake na kuongeza kuwa, “msaada huo umekuja wakati muafaka kwetu huku tukijitahidi kuboresha mazingira ya kujifunzia mashuleni,”

Kizigo alibainisha kuwa madawati 100 yaliyotolewa na benki katika wilaya yake yatasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri zaidi.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad