AKU yajivunia chachu ya mabadiliko ya wahitimu sehemu za kazi - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 21, 2023

AKU yajivunia chachu ya mabadiliko ya wahitimu sehemu za kazi

 *Yaahidi kuendelea kutoa elimu bora kutokana na mahitaji yaliyopo kwenye jamii.


Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Manfredo Fent amesema kuwa Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan wanatakiwa kwenda kuwa sehemu ya chachu ya mabadiliko katika kuhudumia Jamii.

Balozi Fent ameyasema hayo kwenye Mahafali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan yaliyofanyika jijini Dar es Salaam amesema kuwa kuhitimu kwao ndio inakuwa tegemeo katika kufanya mabadiliko sehemu za kazi zao.

Amesema Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) imekuwa iktenga fedha kwa ajili ya maendeleo katika sekta ya Afya na Elimu ili kutatua changamoto katika utoaji wa huduma kwenye jamii

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Tanzania(AKU) Dk.Eunice Pallangyo amesema Chuo hicho Khan kuwa wahitimu wanaotoka katika Chuo ni watu wanaokwenda kufanya mabadiliko sehemu zao za kazi.

Wanafunzi 400 wamehitimu katika vyuo vya Aga khan vilivyopo katika nchi za Afrika Mashariki, ambapo 198 kutoka Kenya, 136 kutoka Uganda na 65 kutoka Tanzania.

Amesema namna Chuo kinavyotoa elimu ndo inafanya wahitimu kwenda na mabadiliko kutokana na mitaala inayotolewa inaendana na nyakati za sasa.

Amesema kutoa Chuo Kikuu cha Aga Khan katika kozi zao wanatoa kulingana na wanafunzi wanachokihitaji ambapo ndio wanakuwa watu kufanya mabadiliko ya kwenda kutoa huduma bora kwenye jamii.

Pallangyo wamebaini kuwa kufundisha pekee sio suluhisho bali kuona wanaofundishwa masomo wanakwenda kutoa matokeo chanya katika utoaji wa huduma kwa jamii katika kutatua changamoto kutokana na maeneo yao ya kazi.

Amesema kazi ya Wahadhiri ni nyepesi kutokana na kusikiliza zaidi wanafunzi kile wachokuja nacho ambapo wakati wanahitimu matarajio yao yanafikiwa.

Aidha amesema katika mahafali hiyo kwa Tanzania kwa mara ya kwanza wamehitimu wengi ikilinganishwa na miaka ya hivi karibuni.

Hata hivyo amesema Chuo Kikuu cha Aga Khan kitaendelea kutoa elimu bora kutokana kadri ya mahitaji yanavyohitajika katika jamii.

"Aga Khan tunajivunia katika kutoa elimu bora inayoendana na mahitaji katika jamii kwenda kutatuliwa changamoto.


Baadhi ya Matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye mahafali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijijoni Dar es Salaam.
Balozi wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania na Jumuiya ya Umoja wa Nchi za  Afrika Mashariki Manfredo Fent akizungumza katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Aga Khan Dk.Eunice Pallangyo akizungumza baada ya kuahirishwa mahafali katika Chuo hicho jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad