HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 26, 2023

𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗠𝗜𝗔𝗞𝗔 2 𝗬𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔, 𝗚𝗔𝗜𝗥𝗢


Mkuu wa Wilaya ya Gairo ndugu Jabiri Makame amesema Wilaya ya Gairo ni Moja ya Wilaya zilizopendelewa sana katika kipindi Cha 𝗠𝗶𝗮𝗸𝗮 2 𝘆𝗮 𝗨𝗼𝗻𝗴𝗼𝘇𝗶 𝘄𝗮 𝗠𝗵𝗲. 𝗗𝗸𝘁 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻, 𝗥𝗮𝗶𝘀 𝘄𝗮 𝗝𝗮𝗺𝗵𝘂𝗿𝗶 𝘆𝗮 𝗠𝘂𝘂𝗻𝗴𝗮𝗻𝗼 𝘄𝗮 𝗧𝗮𝗻𝘇𝗮𝗻𝗶𝗮.

Akizungumza katika Mkutano wa Maadhimisho ya Miaka 2 ya Uongozi wa Rais Samia, DC Makame amesema Wilaya ya Gairo imetekeleza miradi yenye thamani ya zaidi Bilioni 30 katika Sekta zinazogusa maisha ya Wananchi zikiwemo Sekta ya Afya, Maji, Barabara, Elimu, Kilimo na Utawala Bora. Miradi iliyotekelezwa ni pamoja na Mahakama ya Wilaya, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Hospitali ya Wilaya, Vituo 2 vya Afya, Zahanati 8, barabara za lami na zege, madarasa 79, miradi ya Maji Vijiji na mjini nk.

Kwa upande wake Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Gairo Danistan Mwigoha alieleza Mbunge wa Jimbo la Gairo Mhe. Ahmed Shabiby kupitia Ofisi ya Jimbo imetumia zaidi ya milioni 120 kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba Mbunge wa Jimbo hilo anaendelea kufanya jitihada za kutafuta fursa mbalimbali za Maendeleo kwa ajili ya Jimbo la Gairo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo ndugu Dastan Mwendi naye alieleza kuwa, Rais Samia ameitendea haki Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Wilaya ya Gairo, kwani Wilaya ya Gairo inapiga hatua za Maendeleo kwa Kasi kubwa katika Sekta mbalimbali za huduma za Kijamii, na kuwataka Watendaji wa Serikali kwenda na Kasi ya Rais Samia ili kukidhi matarajio ya Wananchi.

















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad