HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2023

Waziri wa Utalii mgeni rasmi Kilimanjaro International Marathon 2023

 

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mbio za Kilimanjaro International Marathon zinazotarajiwa kufanyika Moshi, mkoani Kilimanjaro, Februari 26, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wandaaji wa mashindano hayo, tayari Waziri Mchengerwa amethibitisha kushiriki hafla hiyo ambapo anatarajiwa kuongozana na viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa wa Kilimanjaro na wa ngazi ya Kitaifa katika shughuli hiyo.

"Wakati wa hafla hiyo, Waziri Mchengerwa anatarajiwa kuanzisha rasmi mbio za kilomita 42 na zile za kilomita 21 na kisha yeye mwenyewe kushiriki mbio za kilomita 5 za Granda Malt”, imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa matayarisho yote yameishakamilika na kwamba maonyesho maalaum yajakulikanayo kama Kili Expo yanayotangulia tukio la marathon na ambayo yanafanyika kwa msimu wa pili sasa yanatarjiwa kuanza Alhamisi Februari 23, katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

Imeendelea kuelezwa kuwa katika maonyesho hayo wadhamini mbalimbali wa mbio hizo za kimataifa wanatarajiwa kuonyesha bidhaa, huduma na shughuli mbalimbali wanazozifanya kupitia taasisi zao.

Taarifa hiyo pia imeelwza kuwa maonyesho hayo ya siku nne yataenda sambamba na ukusanyaji wa namba na vifaa kwa ajili ya washiriki wa mbio za Kili Marathon katika viwanja vya MoCU, kuanzia siku ya Alhamisi Febuari 23, saa 6 mchana hadi saa 11 jioni, Ijumaa Februari 24, kuaniza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni na Februari 25, kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni.

Aidha waandaaji wametoa wito kwa wanaotarajia kushiriki mbio hizo kuzingatia muda na siku zilizowekwa kwa ajili ya uchukuaji namba, ambapo wale watakaokwenda kuchukua namba na vifaa kwa niaba ya washiriki halisi watatakiwa kuwa na nyraka za uthibitisho kutoka kwa washiriki halisi waliowaagiza ili kuepuka usumbufu.

"Ni matumaini yetu kwamba washiriki watajitokeza kwa wingi ili kuchukua namba na vifaa vyao vya ushiriki kama ilivyoelekezwa maana namba au vifaa havitatolewa siku ya tukio hata kwa wale waliojiandikisha kwa kufuata taratibu zote”, imesema taarifa hiyo.

Aidhaa taarifa hiyo imetoa onyo kali kwa wale wanaotarajia kushiriki kwa kutumia namba ambazo hazikutolewa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa, ambapo wandaaji wamesema watakaobainika wataondolewa kwenye mashindano hayo na kwamba hao ni pamoja na wale watakaobanika kutumia namba za watu wengine sambamba na wale watakaotumia namba za miaka ya nyuma.

"Kamati ya wandaaji pia inatoa onyo kwa wale wanaoendesha zoezi haramu za kuuza tiketi za bandia kwenye mitandao, hawa wanafuatiliwa kwa makini na watakapobainika, hatua kazi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao”, imesema taarifa hiyo.

Wadhamini wa mwaka huu ni pamoja na wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager (kilomita 42), Tigo (kilomita 21), Grand Malt (kilomita 5), ambapo wadhamini wa meza za maji ni pamoja na TPC Sugar, Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies na wasambazji rasmi ambao ni Surveyed Plots Company Limited (SPC), Kibo Palace Hotels, CMC Automobiles, GardaWorld na Keys Hotel.

Mbio hizi huandaliwa na kampuni ya Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions Limited.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad