HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 14, 2023

Mahakama Kuu yatupiliambali kesi na maombi ya Koyi kubaki rais wa TCCIA

 

Na Mwandishi wetu, Dodoma
MAHAKAMAKuu ya kanda ya Dodoma, imetupiliambali kesi ya msingi na maombi ya kisheria ya Rais wa TCCIA Paul Faraj Koyi ambaye aliiomba mahakama arejeshwe kwenye uongozi wake kwa kuwa alisimamishwa urais kinyume na katiba ya TCCIA na pasipo taratibu za msingi kufuatwa.

Bw Koyi aliiambia mahakama kuwa kusimamishwa kwake ni batili na kuiomba mahakama iamuru arudishwe katika nafasi yake.

Baada ya kusikilia hoja za pande zote mbili katika kesi hiyo, Jaji Fatuma Khalfan, alitupiliambali kesi ya msingi na mombi ya kisheria ya mlalamikaji. Jaji Khalfan ilisema ameridhika chemba ilimsimamisha Koyi kwa kutuata tararibu na katiba yake.

Karibu na mwishoni mwa mwaka jana, TCCIA alieleza kuwa “hivi karibuni kumekuwapo na mivutano ya kimamlaka na kiutendaji kati ya Rais wa Chemba, Bw Koyi na vyombo vingine vya Chemba na pia walioshika nyadhifa mbalimbali za Chemba pamoja na wajumbe wa Bodi na Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba. Mivutano hiyo imesababisha kujitokeza kwa tuhuma mbalimbali dhidi ya Bw Koyi.”

Kwa sababu ya tuhuma hizo NEC ya TCCIA ilikutana kwa dharura Jijini hapa tarehe 31 Oktoba, 2022, kwa mujibu wa ibara ya 34 ya katiba ya TCCIA na kuagiza iundwe tume huru ili kuchunguza tuhuma zinazomkabili Bw Koyi. Tume iliundwa tarehe 3 Novemba, 2022 na ilitakiwa kukamilisha kazi yake ndani ya mwezi mmoja.

Katika taarifa yake tume ilisema kuwa baada ya kuzingatia ushahidi kuhusu tuhuma dhidi ya Bw Koyi, “tuhuma dhidi yake zimethibitika.” Taarifa hiyo inaonyesha kwamba haikupewa ushirikiano na Bw Koyi. “Licha ya jitihada za Tume za kumwalika Bw Koyi kufika kwa ajili ya mahojiiano, hakufika na wito wa Tume wa mwisho hakuujibu.”

Tume ilisema kwamba inatambuaa umuhimu wa mtuhumiwa kutoa maelezo yake na kujibu tuhuma zinazomkabili kwa kuzingatia kanuni za utoaji haki bila upendeleo ambayo imeweka umuhimu wa mtuhumiwa kupewa nafasi ya kusikilizwa. “Kwa kuwa Bw Koyi hakuonyesha ushirikiano licha ya kuitwa mara mbili, alijinyima haki ya kusikilizwa mbele ya Tume. Hivyo, Tume ililazimia kutoa maoni yake kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana,”inasema ripoti ya Tume.

“ Tume inapendekeza NEC ipeleke pendekezo katika Mkutano Mkuu wa Chemba (AGM) la kupima na kuamua iwapo Bw Koyi bado ana sifa za kustahili kuwa Rais wa Chemba kwa kuzingatia maslahi mapana ya Chemba na sifa na mwonekano wa ujumla wa Chemba machoni mwa wananchi na wadau mbalimbali ndani na nje ya nch,” ripoti inasema.

Haijajulikana Mkutano Mkuwa wa TCCIA utaitishwa lini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad