HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 20, 2023

HAKUNA SABABU YA KUENDELEA KUKATA MITI HIVYO....... KAMA KUNA ULAZIMA BASI KATA MMOJA PANDA 10 - DC BAGAMOYO.

 


-Aweka wazi mkakati kupunguza vibali kukata miti ili kuchoma mkaa

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

MKUU wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Halima Okash amesema hakuna sababu ya kuendelea kukata miti hovyo huku akieleza kama kuna ulazima wa kukata basi ukikata mti mmoja utatakiwa kupanda miti mingine 10.

Aidha amesema katika kulinda mazingira na uhifadhi wa mazingira ndani ya wilaya hiyo ameshatoa maelekezo vya kuanza kupunguzwa kwa utolewaji vibali vya kukata miti kwa ajili ya kutengeneza mkaa na watapunguza vibali kwa asilimia 98 na hilo linawezekana.

Okash ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye upandaji miti 1000 katika Shule ya Msingi Kawambwa ambayo imetolewa na Benki ya Standard Chartered ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuendelea kushirikiana na jamii kutunza na kuhifadhi mazingira.Mwaka 2022 walipanda miti 2500 na hivyo hadi sasa inafanya wawe wameshapanda miti 3500 ndani ya wilaya hiyo.

“Najua itatuchoma kidogo lakini haina budi kufanyia kazi hili la vibali, mpaka tutakapofika Julai mwaka huu tutazuia kabisa utoaji vibali kwa ajili ya kukata miti kutengeneza mkaa.Tunayo nishati mbadala ya gesi ya kupikia, hivyo hakuna sababu ya kuendelea kukata miti hivyo na kutengeneza mkaa.

“Hivi karibuni nililetewa orodha ya watu 30 ambao wanaomba vibali vya kukata miti ili wakachome mkaa lakini nimekataa kwasababu hainiingii akilini.Pia nitoe rai kwa taasisi za Serikali Kuu pamoja na serikali ya halmashauri ya Bagamoyo kutenga fedha kwa ajili ya upandaji miti kama ambavyo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan amekuwa akieleza tuhakikishe tunatunza mazingira na vyanzo vya maji.

“Na katika maeneo yote tuhakikishe tunapanda miti na tutunze vyanzo vya maji.Pia nitoe rai wananchi wa Bagamoyo kila kaya ipande miti mitano lakini kila taasisi iliyokuwepo Bagamoyo na Chalinze wapande miti 30 katika maeneo yao,”amesema Okash.

Aidha Okash amesema hivi sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya mabadiliko ya tabianchi hali inayosababisha kukosekana kwa nishati ya kutosha ya umeme, maji , lakini kukosa hewa nzuri

“Sasa hiki tulichokifanya leo cha kupanda miti kinaenda kusaidia kutunza mazingira yetu lakini wanafunzi tuliokuwa nao hapa tunawafundisha bado wakiwa wadogo kuona umuhimu wa kutunza mazingira wanapokuwa majumbani kwao.Tunafahamu ulezi wa watoto unaanzia chini , mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

“Sasa tunaonesha wetu namna ya wao kuanza kupanda miti wakiwa wadogo hata wanapokuwa watakuwa mabalozi wazuri katika utunzaji wa mazingira katika maeneo yetu.Miti hii iliyopandwa tuitunze na tuwe mabalozi na mimi mti wangu nitaendelea kuutunza.”

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Herman Kasekende amesema benki yao imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka 100 na imekuwa inajikita zaidi kwenye kuhakikisha wanafanya kazi na jamii katika shughuli mbalimbali ikiwemo ya mazingira.

Hivyo amesema kutokana na na mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira wameona haja ya kuchukua hatua na wanakwenda sambamba na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya CCM pamoja na muelekeo wa dunia kwa ujumla katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Hapa Bagamoyo mata mwisho tulifanya kazi na Waziri Selemeni Jafo katika mkakati mzima wa kutoshe miti ili kufikia lengo la kuotesha miti milioni 13 na tumehamasishwa na tunaendelea kufanya hivyo kwasababu tunadunia moja hatua dunia nyingine.Hivyo tunahamasishwa kushirikiana na jamii tunatunza mazingira,”amesema.

Awali Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo mkoani Pwani Mwalami Mkenge amesema anatambua suala la mazingira ni muhimu sana katika nchi yetu kwa sasa , hata Ilani ya CCM ya Uchaguzi mkuu ya CCM mwaka 2020-2025 imezungumzia kwa undani kuhusu ulinzi na uhifadhi wa mazingira.

Amesema Standard Chartered wamefika kwenye Wilaya ya Bagamoyo katika shughuli maalumu ya kupanda miti, hivyo ametumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa jambo hilo na kuwaomba waendelee na wasiishie tu kwenye Shule ya Msingi Kawambwa ambayo iko Kilomo bali waende kupanda miti kwenye maeneo mengine ya Bagamoyo kwani kazi wanayoifanya ni kazi ya Mwenyezi Mungu.

“Miti inafaida nyingi sana , inatuletea kivuli, inatuletea matunda, inatuletea mvua , kwa hiyo upandaji miti huu ni muhimu sana , kuja kufanya shughuli hii katika shule ya msingi ni jambo nzuri kwani linafundisha watoto wetu nini cha kufanya katika utunzaji mazingira na watoto ndio wanatakiwa kupewa mafunzo kuhusu utunzaji mazingira.”




MKUU wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Halima Habib Okash akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla upandaji miti 1000 katika Shule ya Msingi shukuru Kawambwaa mwishoni mwa wiki,Kilomo Wilayani humo mkoani Pwani.


Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Herman Kasekende akizungumza mbele ya Wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla upandaji miti 1000 katika Shule ya Msingi shukuru Kawambwaa mwishoni mwa wiki,Kilomo Wilayani humo mkoani Pwani.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shukuru Kawambwa akieleza mambo mbalimbali ya shule hiyo zikiwamo changamoto mbalimbali zinazohitaji kutatuliwa,mbele ya wageni waalikwa kabla ya kuanza zoezi la upandaji miti 1000 katika shule hiyo.

Sehemu ya Meza kuu

MKUU wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Halima Habib Okash akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Herman Kasekende

Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mhe.Mwalami Mkenge akizungumza jambo mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo ya upandaji miti 1000 katika shule ya Msingi Shukuru Kawambwa iliyopo Kilomo,Bagamoyo mkoani Pwani

Diwani wa Kata ya Kilomo Mhe.Salumu Mikugo akizungumza kwenye hafla hiyo






Wageni waalikwa mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakizungumzwa kwenye hafla hiyo.

MKUU wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani Halima Habib Okash na Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered Herman Kasekende kwa pamoja wakishiriki kupanda mti katika shule ya Msingi Shukuru Kawambwa iliopo Kilomo,Bagamoyo mkoani Pwani
Tumeishapanda na sasa tunamwagilia






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad