HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 23, 2023

DHIBITINI UVUJISHWAJI WA SIRI NA NYARAKA ZA SERIKALI : SILINDE

 

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde akizungumza na Makatibu Tawala, Wakuu wa Idara katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti uvujishaji wa siri na nyaraka za Serikali Februari 23, 2023 Jijini Dodoma
\


NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia elimu Mhe. David Silinde amewataka Makatibu Tawala, Wakuu wa Idara katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kudhibiti uvujishaji wa siri na nyaraka za Serikali kwakuwa suala hilo bado ni changamoto.

Mhe. Silinde amesema hayo Februari 23, 2023 Jijini Dodoma wakati akifungua Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu Sekretarieti za Mikoa na Mmlaka za Serikali.

Amesema, hali ya utunzaji wa nyaraka hauzingatiwi kama inavyotakiwa katika maeneo wanayosimamia.

"Bado kuna baadhi ya watumishi mnaowasimamia wanabeba majalada ya siri yakiwa hayajafunika, wengine wanakwenda na nyaraka za Serikali nyumbani"

Amefafanua kuwa hali hiyo husababisha usalama wa nyaraka za Serikali kutozingatiwa na hivyo kuhatarisha ustawi wa Taifa.

Mhe. Silinde amewataka maafisa hao kudhibiti suala hilo na hasa zama hizi za utandawazi kuwa mstari wa mbele kutunza siri za Serikali.

“Mmeaminiwa nendeni mkadhibiti uvujishwaji wa siri za Serikali katika zama hizi za utandawazi muwe mstari wa mbele katika kuzitunza,”amesisitiza

Ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kuongeza uadilifu katika utumishi wa umma na hasa kwa watumishi wa Mikoa na Halmashauri mnaowaongoza na kuwasimamia.

Ameongezea kuhusu ukusanyaji mapato, Mhe. Silinde amewataka watendaji hao kuhakikisha wanaibua vyanzo vipya na kuendelea kupanga rasilimaliwatu katika ukusanyaji wa mapato na wakati mwingine kushauri namna nzuri ya kupata rasilimali watu ili kusaidia kukusanya mapato katika mazingira yenye uhaba wa watumishi.

Akizungumzia kuhusu taratibu za uendeshaji wa mashauri ya nidhamu kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, amesema baadhi yamekuwa hayahitimishwi kwa wakati au watumishi kutokupewa fursa ya kujitetea kwa mujibu wa kanuni na hivyo kutowatendea haki.

Amesema Serikali ilianzisha utaratibu wa kufuatwa katika kushughulikia masuala ya nidhamu kwa watumishi wa Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“ Serikali imekuwa ikipoteza fedha nyingi katika kushughulikia masuala ya nidhamu za watumishi hususani kwa yale ambayo wakati wa kushughulikiwa hayakufuata taratibu za uendeshaji"

Amefafanua watumishi waliorejeshwa kazini baada ya kuonekana kuwa taratibu hazikufuatwa ili hali kiuhalisia makosa ya mtumishi huyo yapo lakini wapo watumishi walioonewa kwa sababu ya utashi wa Afisa Utumishi anayeshughulika na suala lake maana baadhi ya mashauri hayahitimishwi,”amesema.

Amewataka watendaji hao kusimamia suala la maadili hasa mavazi kwa kuwaelekeza watumishi kuzingatia Waraka wa Utumishi wa Umma Na.3 wa mwaka 2007 unaohusu mavazi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Idara ya Serikali za Mitaa TAMISEMI Bi. Angelista Kihaga amesema kikao hicho kitawasaidia maafisa hao kubadilishana uzoefu, kupata mafunzo yatakayo ongozwa na wataalum kutoka Wizara na Taasisi za Serikali na kuamini kuwa watakapotoka hapo wataenda kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad