HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 28, 2023

DC KIBAHA KUSHIRIKINA NA WAALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ILI KUPANDIASHA UFAHULU

 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha  Nickson akizungumza kwenye Kongamano hilo leo Februari 28
Baadhi ya waalimu wakuu na wadau mbalimbali waliohudhuria kongamano hilo

Na Khadija Kalili, KIBAHA
MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amtoa hamasa ya kuwatunuku viwanja na fedha waalimu Wilayani hapa huku lengo likiwa kutia hamasa ya kujenga ari ya kupandisha kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.

DC huyo amesema haya leo kwenye kongamano la kupokea taarifa ya elimu ya Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Mji Kibaha lililofanyika leo asubuhi Februari 28 Mkoani Pwani.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa waalimu watakaofanya vizuri watatunukiwa zawadi ya Viwanja ambapo hii haitaangalia ni ufaulu wa masomo gani na kwa kuanzia wataanza na viwanja 20 ambavyo vitakua katika maeneo mazuri na yenye miundo mbinu yote.

"Tutatoa zawadi kwa shule zenye kutoa matokea mazuri pia nawaagiza waalimu mkawahibike kwa kuwafuatilia wanafunzi kwa kuzungumza nao kwa ukaribu hii itasaidia sana kugundua mahali ambapo mwanafunzi anakumbana na changamoto na kuweza kupata utatuzi wake" amesema DC Nicki.

Amesema kuwa pia watatoa zawadi kwa walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi hasa ikizingatiwa Kibaha ni Wilaya ya Viwanda hivyo uhitaji wa ufaulu wa masomo haya ni wajuu ili kuweza kukidhi maendeleo katika siku zijazo kwa sababu hivi sasa dunia inaendeshwa na Sayansi na Hisabati hata katika maisha ya kawaida hivyo haya masomo ni muhimu katika maisha ya mwanadamu.

Wakati huohuo ametoa wito kwa wazazi kujenga mahusiano ya karibu na waalimu wa watoto wao kwani itasaidia kuona namna ya kuweza kumkwamua mwanafunzi pale alipokwama ikiwa ni pamoja na kuwataka wazazi kuhudhuria mikutano ya shuleni na kuwatimizia wanafunzi mahitaji yote ya shule na kukagua maendeleo yao ya kila siku ya shule.

"Kila mzazi ahakikishe mtoto wake anavifaa vyote vinavyohitajika shuleni, fuatilieni marafiki anaoongozana nao na pia kuasimamia kuwa na marafiki wazuri na kuhakikisha anafanya mazoezi yote ya shule huu ni wajibu wenu" amesema DC Nikki.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa ametia amti kuwa kuanzia sasa kila shule ijiwekee wastani wa ufaulu wa daraja C kuanzia lei hii ikiwa na lengo la kuongeza ufaulu wa Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Afisa Elimu Wilaya Kibaha Rosemary Msesi amesemamkuwa Halmashauri ya Mji Kibaha ina jumla ya Shule 128 kati ya hizo 84 Shule za Msingi na 44 ni za Sekondari katika Shule 128 za Serikali 63 na 65 ni za binafsi na mashirika ya dini.

Amesema kuwa changamoto walizonazo ni pamoja na uhitaji wa vyumba vya madarasa , matundu ya vyoo kwa wanafunzi wa kike(144) na matundu kwa wanafunzi wa kiume (112) na waalimu wa kike(28) na kiume(23),majengo ya utawala, nyumba za waalimu (465) mabweni (12) ,bwalo (16),maktaba (18),maabara ya Kemia (4)Maabara ya Biologia (7), Maabara ya Fizikia(5), Maabara ya Kilimo moja Maabara ya Jiografia (16)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad