HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 16, 2023

DC KIBAHA ATAKA ELIMU ITOLEWE KA JAMII KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO

 

DC wa Wilaya ya Kibaha Nickson John akisisitiza jambo kulia ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Peter Nsanya na kushoto ni Johnson Mndeme kutoka Wizara ya Afya
Kutoka kushoto ni Faith Mamkwe na Afisa Mawasiliano ya magonjww ya dharura Jaliath Rangi wote kutoka WHO.


Na Khadija Kalili Kibaha 
 MKUU wa Wilaya ya Kibaha Nickson John ameitaka Kamati ya magonjwa ya milipuko kutoa elimu juu ya magonjwa kulingana na mila desturi na tamaduni za eneo husika.

Ameyasema hayo Wilayani Kibaha leo Februari 15 alipokuwa akifungua mkutano wa Kamati hiyo inayoundwa na wanajamii, wataalamu wa afya, viongozi wa dini na kamati ya usalama ya Wilaya.

John amesema kuwa kwa kuzingatia hilo itasaidia kukabili magonjwa ya mlipuko kwa kutoa elimu juu ya kukabiliana na magonjwa hayo.

Kwa upande wake Johnson Mndeme kutoka Wizara ya Afya Idara ya Kinga sehemu ya afya kwa Umma amesema kuwa uundaji wa Kamati za Risk Communication and Community Engagement (RCCE) ambazo ni Kamati za Uelimishaji na Uhamasishaji wa Jamii juu ya kupambana magonjwa ya mlipuko ambapo Kamati zimeundwa katika ngazi ya Wilaya hadi Mkoa kufuatia usimamizi wa Wizara ya Afya pamoja na ufadhili wa WHO.

Mndeme amezitaka Kamati hizo kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa jamii nana ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko pindi yanapotokea pamoja na kutoa elimu juu ya kukabiliana nayo ikiwa ni pamoja na kukanusha kauli potofu kwa jamii kama jinsi ilivyotafsiriwa chanjo ya Uviko 19 kuwa mtu akochanja atapatwa ma madhara kauli ambazo ziliwayumbisha wana jamii na kusababisha kuogopa kupatachanjo.

Mndeme amesema kuwa endapo elimu ya kutosha itatolewa mapema magonjwa hayo hayataenea na kuipunguzia gharama serikali kutibu wananchi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Peter Nsanya amesema kuwa wanakamati wanapaswa kutoa elimu ya kupambana na magonjwa mbalimbali ndani ya jamii.

Nsanya amesema kuwa jamii ihamasishwe kujikinga na magonjwa mbalimbali kwa kupata chanjo na kuyakabili magonjwa ya mlipuko pindi yanapotokea ambayo yanaleta athari kwa muda mfupi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad