HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 7, 2023

BILIONI 14 ZILIVYOJENGA SHULE MPYA ZA SEKONDARI 11 NA VITUO VYA AFYA 12 RUVUMA

 

Bilioni 14 zajenga shule mpya 11 na vituo vya afya 12 Ruvuma SERIKALI ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 14 kujenga shule mpya za sekondari 11 na vituo vya afya 12 mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema Mkoa umefanikiwa kujenga shule hizo mpya katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma kwa gharama ya shilingi Bilioni 7.7.

“Ujenzi huu unajumuisha shule ya Mkoa ya Wasichana inayojengwa eneo la Migelegele Kata ya Lwinga katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwa gharama ya shilingi bilioni nne’’,alisema Kanali Thomas.

Hata hivyo amesema Mkoa umefanikiwa kujenga vyumba vya madarasa 792 elimu msingi na sekondari yakijumuisha madawati, viti na meza kwa gharama ya Shilingi Bilioni 14.93

Kwa mujibu wa Kanali Thomas,Mkoa umefanikiwa kujenga mabweni matano ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa gharama ya shilingi Milioni 640 na kwamba Mkoa ulipokea fedha kiasi shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara 23 za Shule za Sekondari kupitia fedha za Tozo na Serikali Kuu.

Akizungumzia kuhusu sekta ya Afya na Ustawi wa Jamii,Kanali Thomas amesema Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga Vituo vya Afya 12 kupitia fedha za Tozo na Serikali Kuu kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 7.8.

Ameongeza kuwa Mkoa umefanikiwa kujenga nyumba tisa za watumishi wa Afya kwa gharama ya shilingi Milioni 856 na kwamba Mkoa umefanikiwa kujenga majengo matatu ya huduma za dharura (EMD) Kwa gharama ya Shilingi Milioni 900.

Kulingana na Kanali Thomas Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kujenga jengo moja la wagonjwa mahututi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwa gharama ya shilingi milioni 250 na kujenga zahanati 21 kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

Hata hivyo amesema Mkoa wa Ruvuma unaendelea na ujenzi wa Hospitali tano za Wilaya ya Nyasa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Halmashauri ya Madaba na Halmashauri ya Songea kwa gharama ya Shilingi bilioni 3.4

Amesema serikali pia inatekeleza mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa awamu ya kwanza katika eneo la Mwengemshindo Manispaa ya Songea kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7.

Amesema ujenzi wa hospitali hiyo unahusisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD), jengo la mionzi na nyumba ya mtumishi na kuongeza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za afya upatikanaji umeongezeka na kufikia asilimia 96.Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza baada ya kukagua mradi wa hospitali ya Madaba wilayani SongeaMradi wa sekondari mpya ya Kungu katika kata ya Nakayaya Halmashauri ya wilaya ya Tunduru ambapo serikali imetoa shilingi milioni 470  kujenga sekondari hiyo 

Mradi wa sekondari mpya ya Lusonga Halmashauri ya Mji Mbinga ambapo serikali imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo
Mradi wa sekondari mpya ya Msisima Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ambapo serikali imetoa shilingi milioni 470 kutekeleza mradi huo
 Jengo la  wazazi katika kituo cha afya Lilambo Manispaa ya Songea ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi milioni 500 kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha afya Jengo la  wodi ya mama na mtoto katika kituo cha afya Masonya Halmashauri  ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo serikali imetoa shilingi milioni 500 kutekeleza mradi  huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad