HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 27, 2023

ASILIMIA 97 WA WANANCHI MKOANI IRINGA NA MAENEO YA PEMBEZONI WANAPATA HUDUMA YA MAJI SAFI

 


Mhandis David Pallangyo akizungumza na wanahabari leo jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (IRUWASA)

Na Janeth Raphael
MAMLAKA  ya maji Safi na usafi wa mazingira (IRUWASA) imevuka lengo la Sera ya maji na ilani ya chama tawala ya kutoa huduma ya usambazaji maji kwa mji wa Iringa na maeneo ya pembezoni inayowafikia wakazi mkoani humo kwa asilimia 97.

Hayo yameyabainisha leo na Mhandisi David Pallangyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji IRUWASA akiwa Jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoani Iringa.

Mhandisi Pallangyo amesema IRUWASA imefanikiwa kuhakikisha huduma ya maji Mjini Iringa na maeneo ya pembezoni inapatikana kwa wastani wa saa 23 kwa siku na imefanikiwa kuongeza ukusanyaji maduhuli (revenue collection) kwa huduma zilizotolewa kutoka wastani Tshs 770M/= (2020) kwa mwezi hadi 860M/= (2023).

"Hali hii inaiwezesha IRUWASA kuweza kugharamia kwa kiasi kikubwa uendeshaji wa Taasisi tumefanikiwa kupunguza kiasi cha maji yasiyolipiwa (NRW) kwa upande wa Iringa Mjini kutoka wastani wa 24.6 (2020) hadi wastani wa 22.52% (mwezi Desemba, 2022), na idadi ya wateja/maunganisho ya Majisafi imeongezeka kutoka 28,133 (2020) hadi 40,549 (Desemba, 2022)" - Mhandisi Pallangyo

Aidha IRUWASA imefanikiwa katika eneo la TEHAMA kwa kufunga mita za malipo kabla (prepaid water meters) kwa wateja 6,752 na kuwa Mamlaka inayoongoza nchini kwa kufunga mita nyingi za maji za malipo kabla na imendelea kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Miji ya Ilula na Kilolo pamoja utekelezaji wa mradi wa Isimani-Kilolo ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2023 .

Hata hivyo Mhandisi Pallangyo amesema pamoja na mafanikio hayo IRUWASA inakabiliwa na changamoto mbalimbali pamoja na mipango ya utatuzi: -Uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji, shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika vyanzo vya maji kama vile kilimo, ufyatuaji wa matofali, mifugo, ukataji miti, uchimbaji wa mchanga/mawe vimekuwa changamoto kubwa kwani vimekuwa vikipelekea kupungua kwa kina cha mto Ruaha mdogo hasa wakati wa kipindi cha kiangazi.

"Kikosi kazi kimeundwa kikishirikisha wajumbe kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Ofisi ya Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kwa ajili ya kusimamia shughuli za utunzaji wa vyanzo vya maji. Kikosi kazi hiki, kinatoa elimu juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji, kinasimamia shughuli za kupanda miti rafiki wa mazingira, kufuga nyuki na kusimamia utekelezaji wa sheria za mazingira." Amesema Mhandisi Pallangyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad