Benki ya NMB imepata nafasi ya kutembelewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum - Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika ofisi zao za Makao Makuu jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa NMB - Ruth Zaipuna aliembatana na Afisa Mkuu wa Fedha
NMB - Juma Kimori, amempokea Mhe. Gwajima na kumuelezea kuhusu
masuluhisho yanayogusa moja kwa moja makundi mbalimbali katika jamii.
Lakini
pia, aliahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha masuluhisho yao
yanakuwa chachu ya maendeleo kwa makundi yote katika jamii kwa kuendelea
kuwekeza kwenye teknolojia na ubunifu.
Katika salamu zake, Mhe.
Gwajima alimpongeza Afisa Mtendaji Mkuu wetu pamoja na uongozi mzima wa
Benki wa NMB kwa mafanikio waliyoyapata, na kuahidi kuna balozi mzuri
kufikisha fursa zinazotolewa na benki hiyo kwa wananchi ili waweze
kujijenga kiuchumi.
No comments:
Post a Comment