HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 29, 2023

FEZA YAONGOZA MATOKEO KIDATO CHA NNE YAFAULISHA DIVISION ONE WANAFUNZI WOOTE

  

Baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne na Baraza la mitihani la Tanzania (NECTA), Shule ya sekondari ya Feza Boys imefanikiwa kuongoza kwa ufaulu wa juu ambapo wanafunzi wote 69 wamefanikiwa kupata division one, kati ya hao, wanafunzi 44 wamepata division 1.7 huku wanafunzi 15 katika masomo yote wamepata alama A.

Hii ni kutokana na juhudi za serikali ya awamu ya sita kupitia wizara ya elimu, kuweka mazingira mazuri na wezeshi hasa katika kutoa ushirikiano mashuleni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

Akizungumza na waandishi wa habari le jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Taluma wa shule ya Feza Boys Richard Mahina, amesema wanafunzi hao walipokua kidato cha pili walifanikiwa kuingia kwenye 10 bora katika mtihani wa Taifa mwaka 2020 ambapo wameendeleza ubora wao mpaka kufikia kidato cha nne.

"Ufaulu huu ni mzuri sana, ni fahari kubwa sana kwetu kama walimu,kama nchi yetu na jamii kwa ujumla kwasababu kikubwa unachotakiwa kwa mwalimu ni ufundishe na utoe matunda yaliyobora "

Pia kutokana na Baraza la mitihani la Tanzania, NECTA kusitisha utaratibu wa kutangaza shule 10 bora na wanafunzi bora kwa matokeo ya kidato cha nne kwa sababu iliyoelezwa kwamba ni utaratibu usio na tija, Mhina amesema wameupokea vizuri uamuzi huo na wapo pamoja na serikali.

"Ni kweli wanafunzi wanasoma katika mazingira tofauti, kikubwa ni kwamba wanafunzi wanasoma vizuri na bahati nzuri wanafunzi wetu wamefanya vizuri sana hivyo tupo pamoja na serikali uamuzi waliouchukua ni mzuri na sisi tunauunga mkono "

Maina amewapongeza wanafunzi wote wa kidato cha nne wote 69 ambao wamejitahidi kwa kuhakikisha wanakuwa na uthubutu katika masomo yao na kupeleka kutoa matokeo mazuri shuleni hapo.

Aidha Maina amewashukuru wazazi wa wanafunzi hao lakini pia uongozi wa feza schools kwa kuwapa ushirikiano hadi kupelekea kupata matokeo hayo huku akiwataka walimu wengine kuchukua mfano huo wa walimu wa mwaka jana.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Feza Boys, Bussury Omary amesema walitarajia wanafunzi wao wangefanya vizuri kutokana na juhudi walizokuwa nazo katika kutaka kujifunza na kuwa na uelewa wa kutosha.

"Walituaminisha kwamba wanaweza na kweli wamefanikiwa, tunawashukuru wazazi, uongozi, walimu na wanafunzi wenyewe kwani wanafunzi hawa walichokifanya kinahitaji heshima ya juu, pia tunaishukuru serikali kwa kuondoa utaratibu wa kutaja shule na mwanafunzi bora kwani inaweza ikasaidia sana kuondoa wizi kwenye mitihani "

Omary amesema wanafunzi wote ambao wamefaulu wanawapatia zawadi kutokana na ufaulu wake lakini pia walimu ambao wamefanya wanafunzi hao kupata ufalu huo wanapewa pongezi zao.

Naye Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Feza Boys aliwapongeza wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2022 kwa ufaulu wao mzuri, hali inayowapelekea wao kupata morari ya kusoma zaidi na hata kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwaka huu.

Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Sekondali Fedha Boys'Bussury Omary akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,baada ya shule yao kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa kidato cha nne mwaka jana,kushoto ni mwalimu wa taaluma wa shule iyo,Richard Maina.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Feza boys wakishangilia baada yabkutangazwa kwa matokeo ya kidato cha nne na shule hiyo kuongoza kwa kufaulisha division one kwa wanafunzi woote waliomaliza shuleni hapo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad