HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 1, 2022

WAKE WA VIONGOZI NGAZI WILAYANI SONGEA WAKABIDHIWA MITUNGI YA ORYX GASI 600

 

 Na Mwandishi Wetu,Ruvuma

WAKE wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma wamepatiwa mitungi ya gesi 600 pamoja na majiko yake kutoka Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd  ikiwa ni mkakati wa kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini huku pia mwanamke wa Tanzania akiendelea kuondolewa changamoto ya kutafuta kuni na mkaa kwa ajli ya kupikia.

Majiko hayo yamekabidhiwa leo Novemba 30 mwaka 2022 na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite mbele ya viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvua wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.

Akizungumza baada ya kupokea majiko hayo kwa niaba ya wake wa viongozi ,Waziri Mhagama amesema katika  kampuni ambazo zinatoa huduma ya gesi ya kupikia majumbani Oryx inaongoza kwa kubadilisha maisha ya wanawake wa maeneo mbalimbali nchini kwa kuwapatia majiko ya gesi na lengo kubwa ni kuhifadhi mazingira na kuongeza Mkurugenzi wa Oryx sio mtanzania lakini amemsikiliza Rais Samia na ameona haja ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kulinda na kuhifadhi mazingira.

Amesema uharibifu wa mazingira umekuwa chanzo cha madiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha mvua kuwa chache kutokana na miti kuendelea kukatwa, hivyo kupitia majiko ya gesi yaliyotolewa na Oryx yanakwenda  kusaidia kuihifadhi mazingira na hivyo mvua kuendelea kunyesha na wananchi kupata mazao.

“Dawa ya kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni kutunza misitu na dawa ya kutunza mazingira ni moja tu ambayo ni kutumia nishati ya gesi , mtungi ambao thamani yake ni zaidi ya Sh.70,000 lakini kwa wanawake wa Peramiho imetolewa bure tena mtungi ukiwa na gesi iliyojaa.Mitungi na majiko ya gesi ambayo imetolewa leo ndio zawadi ya Kristmass kwa wanawake wa viongozi,amesema Waziri Mhagama.

Ameongeza siri mojawapo ya kuonekana maisha yako mazuri ni pamoja na kutumia gesi, jambo la msingi tu ni kuweka fedha kidogo kidogo ili gesi inapoisha inanunuliwa nyingine huku akisisitiza kanawapenda sana wanawake wa viongozi wa Jimbo la Peramiho na ndio maana ameamua kuwatafutia majiko hayo ili nao wawe wanapika kwa raha.

“Tunawashukuru sana Oryx kwa zawadi hii ya kwa wanawake wa viongozi.Zawadi hii ambayo tumepewa inakwenda kubadilisha maisha yako,”amesema Waziri Mhagama huku akitumia nafasi hiyo kueleza baada ya Rais Samia kuupiga mwingi kwenye maeneo mbalimbali kwa kuimarisha uchumi yeye kama mbunge wa jimbo la Peramiho lengo lake sasa ni kuona wanaimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na hivyo ametoa rai kwa wadau  kuendelea kushirikiana na wananchi wa Peramiho kujenga uchumi kwani huo ndio mpango wake kwa sasa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite alisema wataendelea kufanya uwekezaji mkubwa nchini Tanzania kwa makundi mbalimbali ya wananchi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya gesi safi ya LPG ambayo ni suluhisho la kuondoa matumizi ya kunina mkaa, hivyo basi kuboresha afya ya jamii na kulinda mazingira.

“Wakati wa kongamano la nishati safi kwa wote lililoandaliwa na Wizara ya Nishati na kufanyika jijini Dar es Salaam Mwezi wa Novemba 1 na 2, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alieleza wazi lengo lake la kuona asilimia 80 hadi 90 ya idadi ya watu wa Tanzania kupatiwa ufumbuzi wa kupika kwa nishati safi ndani ya miaka 10 ijayo.

“Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd, katika kuunga mkono lengo hilo adhimu, imeongeza juhudizake kwa kusaidia jamii mbalimbali kubadilisha matumizi yasiyo ya kiafya ya kuni na mkaa kwakutumia LPG ambayo ni rafiki kwa mazingira na afya. OGTL inaendelea kuwekeza katika uagizaji, uhifadhi, ujazaji wa gesi kwenye mitungi na usambazaji wa LPG Tanzania nzima, pamoja na Visiwa vyake,”amesema Benoite.

Aidha amesema OGTL huwekeza kila mwaka mamilioni kadhaa ya dola kwenye mitungi mipya inayoingizwa sokoni kila siku na kwamba inatoa . mitungi hii kwa punguzo kubwa, ikigharimia kwa kiasi kikubwa vifaa vya kuanzia vya LPG (Silinda, Gesi, Burner, Trivet) ili kuwezesha wananchi kubadili kutoka kwa nishati za kuni na mkaa hadi kwagesi safi na kufanya gesi ipatikane kote nchini.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini mkoani Ruvuma Mwalimu Neema Maghembe alisema wanamshukuru Mkurugenzi wa Oryx Gas kwa kuwaona akina mama na kusikia kilio chao kwa kuwapatia mitungi na majiko ya gesi kwa ajili ya kupikia.

“Yaani kupika kwa kutumia kuni na mkaa sasa basi tena, Mbunge wetu na Waziri wetu hili ni jambo kubwa na la kihistoria , kwa wanawake wa songea Vijiji kwenye Jimbo la Peramiho akina mama watatuma majiko ya gesi, yale mambo ya umetoka shamba umechoka halafu unahangaika na kuni sasa basi, ni mwendo wa gesi,”alisema Maghembe.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Songea Vijijini Thomas Masolwa amesema kitendo cha Waziri Mhagama kuhakikisha Oryx Gas wanatoa majiko hayo kwa wake wa viongozi ndani ya wilaya hiyo kunakwenda kufanya wake hao sasa wawe wanapika chakula kisasa zaidi na hawatakula tena chakula chenye harufu ya moshi wa kuni na mkaa.

“Mbunge wa jimbo letu la Peramiho na Waziri wetu Jenista Mhagama CCM tunasema wewe chapa kazi, hakuna mbadala wako kwa sasa, tunakuomba endelea kupeleka salamu zetu kwa Mkurugenzi wa Oryx umwabie tunamshukuru sana na jambo hili kubwa ambalo umelifanya linaonesha uhusiano mzuri ulionao kati yako na Oryx pamoja na wadau wengine wa maendeleo.”




Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama(kushoto) na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(katikati) wakimkabidhi mtungi wa gesi wa Oryx Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Juma Nambaila.


Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(kushoto)akimkabidhi mtungi wa gesi  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini Menasi Komba (kulia).Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.


Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Limited Araman Benoite(kushoto) akimkabidhi mtungi wa gesi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini Neema Maghembe(kulia).Katikati ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menemjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Jenista Mhagama.Mtungi huo ni kati ya mitungi 600 iliyotolewa na Oryx Gas Tanzania kwa ajili ya kuwapatia wake wa viongozi kwenye halmashauri hiyo kama mkakati wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kutunza na kulinda mazingira.






Matukio mbalimbali katika picha baada ya mitungi ya Oryx kukabidhiwa kwa wake wa viongozi wa ngazi mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma .Mitungi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Oryx Gas Tanzania Ltd Araman Benoite leo.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad