HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 12, 2022

WADAU WA BAHARI KUTOKA NCHI 15 WANOLEWA, TASAC WAAHIDI KURIDHIA MKATABA WA KIMATAIFA WA BAHARI

 KATIKA kuhakikisha mazingira ya Bahari na maji yanatuzwa wadau wa mazingira kutoka nchi mwanachama 15 wa Afrika wameshiriki katika Warsha ya siku tatu kwaajili ya kukuza uelewa wa pamoja juu ya Mkataba wa kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza katika warsha hiyo leo Desemba 12 jijini Dar es Salaam amesema kuwa Mwitikio wa nchi mwanachama umekuwa mkubwa na ni jambo ambali dunia imeanza kuipa kipaumbele mkataba wa kimataifa kwaajili ya kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha viumbe vitakavyo zaliwa majini vinakuwa hai.

Akizungumzia kuhusiana na Hali ya bahari kwa sasa amesema kuwa Mazingira ya Bahari kwa sasa ni manzuri lakini tahadhari mbalimbali lazima zitolewa kwaajili ya Vizazi vya vijavyo.

"Ifahamike kuwa vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia sera ya uchumi wa bluu, sasa bahari inapochafuka na inapoharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa bluu inakuwa ngumu kwani kwa sababu ya viumbe ambavyo vinafanyika kuwa uchumi vitapotea pamoja na vyombo vya usafiri majini vitaharibika na kushindwa kufanya kazi inayotakiwa."
Amesema Dkt. Possi

Amesema kuwa mkutano huo utatilia mkazo wa uridhiaji wa itifaki ya sheria ya bahari kwaajili ya kuendeleza uelewa mpana wa wadau wote.

Washiriki wa mkutano huo ni Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
(TASAC), Bandari, Taasisi ya Bahari ya Dar es Salaam (DMI) wa wawakilishi wa Nchi 14 za Afrika.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge amesema Shirika hilo limekasimiwa mamlaka ya kudhibiti mazingira ya majini na Maji yanayotokana na uchafunzi wa vyombo vya Usafiri Majini hivyo madhumuni ya warsha hiyo ni uelewa wa pamoja wa Jinsi ya kudhibiti maji, kusimamia masuala ya usafiri majini.

.....kwa kukaa sana yale maji inawezekana kuna viumbe ambavyo vinazaliwa na yale maji yaliyokuwa kwenye meli hakishushwa baharini katika maji ya kitaifa au eneo lolote la bahari kunauwezekano wa kushushwa na viumbe wengine ambao wamezaliwa baada ya yale maji kukaa muda mrefu

Hivyo basi yale maji yakishushwa yanaweza kuzalisha viumbe wengine ambavyo vitakuwa hatarishi kwa uendelevu viumbe ambao wapo baharini na tunavihitaji.

Amesema uchumi wa bluu unaweza usifikiwe kama maji yanakuwa hayadhibitiwi. Kwahiyo hatutaufikia uchumi wa bluu kama mikataba hii hatutairidhia na kuzingatia ni jinsi gani tunaweza kujikinga na hivyo viumbe ambavyo vinaweza kuzalishwa.

Shirika la Kimataifa la Bahari linatoa elimu kwa Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya usafiri kwa njia ya maji, taasisi zinazohusika na masuala ya bahari zimeshiriki warsha hiyo ili kuwa na uelewa wa pamoja ili mkataba utakaporidhiwa na kutengeneza kanuni za Kutumika hapa nchini.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo amesema kuwa maji yanahobebwa na meli yanasaidia meli pale ambapo inakuwa haina mzigo pia ikiwa na mzigo mdogo yanapunguzwa au kuongezwa ili kuweka uzito sawa katika meli na Maji hayo watu wenye meli wamekuwa wakiyamwaga baharini jambo ambalo sio zuri.

"Maji hayo yanaviumbe na mimea ambayo sio asili ya huku kwetu kwa hiyo ikitokea yanamwagwa baharini yatakuwa na viumbe wavamizi wataleta namna tofauti ya kimazingira Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) liliona umhimu wa kuweza kudhibiti hali hiyo kwa sababu kimazingira sio sawa, kinachotakiwa ni kuto kumwagwa baharini kama nchi mwanachama wa IMO tunatakiwa kuridhia mkataba huo ili kuweza kusimamia kuwa haitakiwi ukifika bandarini kumwaga maji inatakiwa kwenda kumwagwa katika kati ya habari ili yasiweze kuleta shida katika eneo letu la mazingira ya maji.

Amesema Kwa Tanzania Sasaivi tupo katika hali nzuri kwa sababu tumeshaanza kuridhia mkataba pia amesema Kama wizara wameshatoa maoni na mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na mkataba huu. Na mpaka sasa wameshaanza kupokea maoni yao.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufungua warsha ya Siku tatu kwa wadau wa Bahari leo Desemba 12 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 12, 2022.
Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 12, 2022.
Baadhi ya wadau wa habari kutoka nchi 15 wakiwa kwenye warsha ya siku tatu wakijadili itifaki ya usimamizi wa habari na mazingira.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad