MSHINDI WA PROMOSHENI YA NMB MASTABATA KOTEKOTE AKABIDHIWA PIKIPIKI JIJINI MWANZA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 2, 2022

MSHINDI WA PROMOSHENI YA NMB MASTABATA KOTEKOTE AKABIDHIWA PIKIPIKI JIJINI MWANZA

 

 Mshindi wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku (kulia) akipokea funguo ya pikipiki kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Baraka Ladislaus wakati wa hafla ya kukabidhiwa. Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya kadi wa NMB – Philbert Casmir.

Mshindi wa Kampeni ya MastaBata KoteKote, Bernard Matiku(wa pili kushoto) akibonyeza kitufe ili kuwapata washindi wengine wa kampeni hiyo. Wakishuhudia; Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Biashara ya Kadi wa NMB- Philbert Casmir, Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa – Baraka Ladislaus(wa tatu kushoto) na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha – Erick Mremi(kulia).

*****************

nne wa promosheni ya NMB MastaBata kwa ajili ya kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za kidijitali umezidi kunoga baada ya kundi la kwanza la washindi 51 wa kila mwezi kupatikana katika droo iliyofanyika kwenye tawi la NMB Kenyatta mkoani Mwanza wiki hii, ambapo 49 walijishindia pesa taslimu TZS 1,000,000 kila mmoja na wawili wakishinda pikipiki aina ya Boxer.

Lengo la kampeni hii ya MastaBata KoteKote ni kuhamasisha matumizi ya kadi ya NMB Mastercard na Lipa Mkononi (Mastercard QR) kwa wateja wetu wanapofanya malipo kwenye manunuzi yao.

Mkazi wa Bunda jijini Mara, Bernard Lucas Matiku alisema ‘Asante sana Benki yangu ya NMB kwa kunizawadia pikipiki, nimeanza vizuri msimu huu wa sikukuu maana sasa sina wasiwasi kuendesha mishe zangu’ baada ya kukabidhiwa pikipiki aliyoshinda katika promotion ya NMB MastaBata KoteKote.

Zoezi hilo lililosimamiwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania limepelekea idadi ya washindi wa kampeni ya NMB MastaBata KoteKote kufikia 225 hadi sasa. zawadi walizoshinda wateja hao kwa siku hii zina thamani ya zaidi ya TZS milioni 55 huku shindano zima likiwa na thamani ya zaidi ya TZS milioni 300.

Zawadi za kila wiki zitakuwepo ambapo jumla ya washindi 75 watanyakua pesa taslimu TZS 100,000 kila mmoja na mmoja zawadi ya Pikipiki (boxer), kwa mwezi jumla ya washindi 98 watanyakua pesa taslimu TZS 1,000,000 kila mmoja huku kila mwezi kukiwepo zawadi ya Pikipiki (Boxer) mbili. Zawadi ya droo ya mwisho ni safari ya siku nne huko Dubai kwa washindi saba na wenza wao.

Endelea kufanya malipo kwa kutumia NMB mastercard au Lipa Mkononi (mastercard QR) ujiwekee nafasi ya kushindia zawadi kibao na #NMBMastaBataKoteKote No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad