HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 9, 2022

KAMPUNI ZA MAFUTA WAKIONGOZWA NA ORYX WAWEKA MKAKATI KUKABILIANA NA MAJANGA

 
Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI Oryx Energies kwa kushirikiana na kampuni nyingine za uagizaji na usambazaji mafuta nchini Tanzania zilizopo eneo la Kurasini jijini Dar es Salaam wameshirikiana kwa pamoja kuendesha zoezi la kukabiliana na janga la moto kwenye maeneo ya shughuli zao huku wakitumia nafasi hiyo kuahidi kuendelea kuimarisha miundombinu ya usalama katika shughuli zao.

Zoezi hilo la kukabiliana na janga la moto limefanyika kwenye leo Desemba 8 mwaka 2022 kwenye Kampuni ya Oryx Energies Kurasini jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na wakurugenzi na maofisa wa kampuni za mafuta chini ya mwavuli wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania(TOAMAC) , Jeshi la Polisi, Jeshi la Zima Moto, wawakilishi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), madereva wa magari ya mafuta, wananchi pamoja na wadau wengine muhimu hasa wanaohusika na kukabiliana na majanga.

Kabla ya kuanza kwa zoezi hilo, ilisikika alamu ya kuashiria hatari , hivyo wafanya wa kampuni ya Oryx pamoja na kampuni nyingine za mafuta walioko katika eneo hilo walikusanyika eneo maalumu na kisha taarifa ikatolewa kuhusu hatari iliyopo na baadae magari ya zima moto, Ambulance na watoa huduma ya kwanza wakawa wamefika eneo la tukio na kuanza uokoaji.Zoezi ambalo limefanyika kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza mbele ya wadau mbalimbali baada ya kumalizika kwa zoezi hilo lililoratibiwa kwa ushirikiano wa kampuni za mafuta zilizopo Kurasini, Mkurugenzi wa Oryx Energies ambaye pia ni Mwenyekiti wa TOAMAC Kalpesh Mehta amesema ni jambo la msingi kujiandaa kwa kukabiliana na majanga katika maeneo ya shughuli zao, hivyo wameamua kuungana na kufanya zoezi hilo.

“Majanga yanayoweza kutokea kwenye kampuni zetu, kwenye shughuli zetu tunazofanya Kigamboni na hapa Kurasini, ni muhimu kuwa na uhakika wa usalama wa kila mtu. Watu wanaoishi maeneo yaliyokaribu na shughuli za mafuta hasa haya maeneo ambayo tumehifadhi mafuta pamoja na maeneo mengine lazima wawe na utayari kukabiliana na majanga yanapotokea. Hivyo nasi kwa nafasi yetu tumeamua kufanya zoezi la kujiandaa ili kujilinda sisi na kulinda majirani zetu,”alisema Mehta.

Aidha amesema wanatambua eneo la Kurasini ndiko iliko Bandari ya Dar es Salaam ambao ni mlango wa uchumi kwa nchi sita ambazo zinaizunguka Tanzania, hivyo lazima wahakikishe kuna usalama wa kutosha na Tanzania ni lazima kuwa na kiongozi wa mfano katika kuhakikisha usalama upo wa uhakika.

Kuhusu ombi la Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zima Moto Maria Luwoga la kuziomba kampuni za mafuta zilizopo Kurasini kushirikiana ili kununua mtambo wa kuzima moto utakaokuwa eneo hilo muda wote, amesema ni wazo zuri hivyo kupitia chama chao wataangalia nini kifanyike.

Kwa upande wake Meneja Operesheni wa Kampuni ya Oil Com Salehe Islam amesema wanavipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha sheria za kukabiliana na majanga zinaheshimiwa na kufuatwa kikamilifu huku akielezea zoezi ambalo limefanyika linaonesha namna walivyoamua kushirikiana kwa pamoja kuwa na mkakati utakaowezesha kujaindaa kukabiliana na majanga.

Awali wake Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zima Moto na Uokoaji Mkoa wa Temeke Maria Luwoga pamoja na kuwapongeza Oryx kwa kuandaa zoezi hilo, lakini ametoa ushauri kwa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania kuangalia uwezekano wa kushirikiana kunununua mtambo wa kuzima moto.

“Nitoe naombi au ushauri hasa kwa Chama Cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania kama itawapendeza kwa kushirikiana na Jeshi la Zima Moto kununua mtambo wa kuzima moto utakaokaa eneo hili la Kurasini kwani hiyo itasaidia kwenye udharura ambao utatokea.Ofisi za Zima Moto ziko Kigamboni mpaka uvuke daraja na nyingine ziko eneo la Mchicha baada ya kuvuka daraja la mfugale.

“Mazingira yetu sisi ya barabara ni ngumu sana kufika kwa wakati na ukiangalia usali wa tukio mafuta, gesi kwa maeneo yetu.Maendeleo ya uchumi hayawezi kupatikana bila usalama , kwa hiyo usalama ndio kipaumbele namba moja , lakini anatamani kuona mazoezi ya kukabiliana na majanga yakiendelea kufanyika mara kwa mara,”alisisitiza.


:Sehemu wa watoa huduma ya kwanza wakiwa wamembeba moja wa majeruhi aliyepatikana kwenye janga la kuzima moto ambalo limetokea eneo la Kampuni ya Oryx iliyopo Kurasini Dar es Salaam.Janga hilo la moto ambalo limetokea ni sehemu ya zoezi la kuzima moto kwenye maeneo ya kampuni za mafuta , lengo likiwa kujiwekea tayari kukabiliana na majanga yakiwemo ya moto.



Baadhi ya waokoaji wakiendelea na zoezi la kukabiliana na majanga katika eneo la Kampuni ya Oryx Energies iliyopo Kurasini jijini Dar es Salaam.Uokoaji huo unafanyika kama sehemu ya kukabiliana na majanga kwenye maeneo yenye nishati ya mafuta ambapo kampuni za uagizaji na usambazaji mafuta nchini chini ya uratibu wa Oryx wameandaa zoezi hilo ambalo limewashirikisha wadau mbalimbali.


Mkurugenzi wa Oryx Energies ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Waagizaji na Wasambazaji wa Mafuta Tanzania (TOAMAC)Kalpesh Mehta akizungumza na wadau mbalimbali wanaohusika na masuala ya kukabiliana na majanga pamoja na wakurugenzi wa kampuni mbalimbali za mafuta zilizopo Kurasini Dar es Salaam jana baada ya kufanyika kwa zoezi la kukabiliana na majanga ambalo limefanyika kwenye kampuni ya Oryx.Ametumia nafasi hiyo kueleza kwamba wadau hao wataendelea kushirikiana katika kuendelea kufanya mazoezi ya kukabiliana na majanga ili kuwa na utayari.(Na Mpiga picha Wetu).



Wafanyakazi wakiendelea kukusanyika eneo la wazi baada ya kusikia alamu ya kuashiria hali ya hatari



Wafanyakazi wa Kampuni ya Oryx wakipewa maelekezo na mmoja ya maofisa wa kampuni baada ya kukusanyika eneo la wazi kutokana na kulia kwa alamu ya hali ya hatarini kwenye eneo hilo.


Baadhi ya wakurugenzi wa kampuni za mafuta, maofisa na wadau mbalimbali wa masuala ya usalama wakifuatilia maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wadau baada ya kumalizika kwa zoezi la kuzima moto lililofanyika kwenye kampuni za mafuta Kurasini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad