BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA KWA WAAJIRI WA NDANI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 4, 2022

BENKI YA CRDB YATWAA TUZO YA MWAJIRI BORA WA MWAKA KWA WAAJIRI WA NDANI

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango (wapili kulia) akimkabidhi tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka kwa Waajiri wa Ndani, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa (wapili kushoto), katika hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. wengine pichani ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi. Jayne Nyimbo.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akihutubia wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki 
 
 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya CRDB, Godfrey Rutasingwa akizunngumza wakati wa hafla ya Utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Benki ya CRDB ilishinnda tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka kwa Waajiri wa Ndani.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa kwenye hafla ya Utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2022 zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na kufanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
Furaha ya Ushindi: Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa ni wenye furaha baada ya kushinda tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka kwa Waajiri wa Ndani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa vipengele mbalimbali vya waajiri bora wa mwaka 2022 wakati wa Hafla ya utoaji tuzo hizo zinazoratibwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) iliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad