HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 22, 2022

WAKULIMA: WANASIASA WANATUONEA WIVU ANAYOTUFANYIA RAIS

 


Na John Walter-Manyara
Wakulima wilayani Babati mkoani Manyara wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia bei ya Mbolea.

Wakulima hao wakiwa Kwenye maandalizi ya kumpokea Rais Samia anayefanya ziara mkoani hapa leo Novemba 22 na 23 wamejitokeza na mabango yaliyoandikwa maneno ya pongezi kwa Rais, ambapo wamesema awali walikuwa wakinunua Mbolea kwa shilingi laki Moja na nusu lakini kwa sasa wananunua kwa 70,000 tu.

Kiongozi wa wakulima hao mkoa wa Wilaya ya Babati Ali Myombo, amesema hawana cha kumlipa Rais Samia ila wataendelea kumuunga mkono hadi 2030.

Amesema kutokana na mambo makubwa wanayofanyiwa wakulima na Rais Samia baadhi ya wanasiasa wanaona wivu na kukosa hoja za kuzungumza kwenye majukwaa.

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua wananchi wengi wanajishughulisha na Kilimo ndio maana imewawekea Mazingira rafiki ya Kilimo.

Amesema katika kuendelea kukipa thamani Kilimo, Rais Samia amejenga Mahusiano mazuri na nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika hivyo kurahisisha wafanyabiashara kuja kununua mazao ya wakulima kwa bei rafiki.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad