WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO, WALIO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI WAASWA KUJIUNGA NA VIKUNDI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 27, 2022

WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO, WALIO KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI WAASWA KUJIUNGA NA VIKUNDI

 
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza wakati wa Kusambaza matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe leo Novemba 26, 2022 jijini Dar es Salaam kwa Wafanyabiashara ndogo ndogo wa Mbagala.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyabiashara ndogondogo na Madereva wa Daladala waliofikisha miaka 50 na Zaidi.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ndogo ndogo na Madereva daladala na Bodaboda wa Mbagala jijini Dar es Salaam leo Novemba 26, 2022 
Mhamasishaji wa Kujiunga na vikundi, Amani Mwinyimkuu akitoa elimu ya jinsi ya kujiunga na Vikundi mbalimbali kwa wafanyakazi wa Sekta isiyorasmi.

Mmoja ya waendesha Daladala akiuliza swali kwa watoa mada wakati wa Usambazaji wa Matokeo ya Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe.

Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo wa Mbagala jijini Dar es Salaam wakimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza wakati wa Kusambaza matokeo ya Utafiti leo Novemba 26, 2022 jijini Dar es Salaam.

WAFANYABIASHARA ndogo ndogo na Waendesha daladala na Bodaboda wameaswa kuunda vikundi ambavyo vitawapa fursa mbalimbali za kujiinua kiuchumi na Kijamii.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza wakati wa Kusambaza matokeo ya Utafiti huo leo Novemba 26, 2022 jijini Dar es Salaam kwa Wafanyabiashara ndogo ndogo wa Mbagala amesema kuwa Waendesha bodaboda itawasaidia kujulikana ni kikundi gani wametokea pale inapojitokeza changamoto kwani wameonekana kuwa na taswira ambayo sio nzuri kwa jamii.

Amesema Utafiti uliofanywa na chuo Kikuu Mzumbe kuanzia Mwaka 2017 katika Sekta ya Usafirishaji na wafanyabiashara ndogo ndogo juu ya kujipatia huduma za hifadhi za jamii na bima ya Afya umeonesha asilimia 68 tuu ndio wamejiunga na vikundi.

Pia amesema kuwa wakijiunga kwenye kikundi chochote itawapa hadhi ya kazi yao kwani watakuwa wanatambulika hadi kwenye serikali ya Mtaa na Kata.

"Waendesha bodaboda hawawezi tena kujiingiza kwenye matendo maovu kwani watakuwa wanajulikana Serikalini na kila mmoja anajua watu wanamjua na wanakuheshimu." Amesema Dkt. Kinyondo

Vikundi pia kwa wafanyabiashara ndogondogo na waendesha daladala amesema vitawasaidia kupata mikopo katika taasisi za kifedha kwani kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi ni nadra kupata mikopo katika taasisi hizo.

Dkt. Kinyondo amesema watu wa sekta zisizo rasmi wanakopa katika taasisi za fedha binafsi na wanariba kubwa kuliko taasisi za fedha ambazo zinaaminika zaidi. "Lakini wakiwa kwenye Kikundi, kikundi kinakuwa Mdhamini mkuu wakiwemo wanakikundi wenyewe..."

Akitolea mfano Waendesha daladala wa Pugu na Wajenzi wa Kata ya Sinza amesema wamejiunga kwenye vikundi na wamepata mkopo kutoka benki na sasa wanaonja matunda ya kuwa na kikundi.

"Kutokana na kuwahamasisha kupitia tafiti tuliyoifanya Mzumbe, Madereva wa Pugu tuliwaunganisha na benki wakakopa na sasa wamenunua Daladala nne ambazo zinawaingizia kipato kama kikundi. Na Wajenzi wa Sinza waliunganishwa na benki waliweza kupata mkopo na sasa wanavifaa vya ujenzi wanaweza kupata tenda mbalimbali za ujenzi." Amesema Dkt. Kinyondo

Amesema vikundi pia vinasaidia katika kutafuta bima ya Afya kwa wanakikundi nirahisi kwa mchakato wake pamoja na gharama ni nafuu, hivyo ameendelea kuwaasa kujiunga na vikundi ili kupata unafuu wa kupata huduma mhimu.

Aidha Dkt. Kinyondo ameeleza kuwa Vikundi vinaweza kuwasaidia kuchangia katika mifuko ya Pensheni ingawa kila mmoja anaweza kuchangia lakini kwa Kikundi ni rahisi zaidi.

Utafiti huo umeonesha kuwa zaidi ya Asilimia 71 ya wafanyabiashara hao hawana namna ya kupata mikopo kwa kuwa hawana maeneo rasmi ya Kufanyia biashara na hawaaminiki kwa kuwa kila siku wanabadilisha maeneo ya Kufanyia biashara.

Kwa Upande wa Amani Mwinyimkuu amesema kuwa kwa wafanyabiashara wa Mbagala bado hawajafanikiwa kuwa na vikundi imara hivyo amewaasa wajiunge na Vikundi ili kuweza kupata fursa mbalimbali.

Katika Usambasaji wa Matokeo ya Utafiti Chuo Kikuu Mzumbe kimewapa viakisi mwanga wafanyabiashara ndogo ndogo na walio katika Sekta ya usafirishaji ambavyo vinaujumbe na Namba za simu za watu wa Mikopo, Bima ya Afya na Mfuko wa Pensheni ambazo zitawawezesha kujipatia fursa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad