VULU ASHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA MWENYEKITI UWT MKOA WA PWANI. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 18, 2022

 VULU ASHINDA KWA KISHINDO NAFASI YA MWENYEKITI UWT MKOA WA PWANI.


- Achaguliwa kwa kura 358, mpinzani wake aambulia kura 38 pekee.

- Wagombea wengine wawili waingia mitini.

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake CCM Mkoa wa Pwani wamemchagua aliekuwa Mbunge wa Viti maalumu Pwani Mhe. Zaynab Matitu Vulu kuwa Mwenyekiti mpya wa UWT Mkoa huo.

Mhe. Vulu ameshinda nafasi hiyo kwa kupata jumla ya kura 320 Kati ya kura 358 zilizopigwa akifuatiwa na Joan Tandau aliepata kura 38 pekee huku wagombea wawili waliokuwa wakiwania nafasi hiyo wakiingia mitini na kupata kura sifuri.

Katika uchaguzi huo idadi ya kura zilizopigwa ni 358 na hakuna kura iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Mhe. Zaynab Matitu Vulu amewashukuru wajumbe kwa Imani kubwa na dhamara waliyompatia ambapo amewaahidi kuendelea kuwatumikia kwa uaminifu mkubwa.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad