UJERUMANI WAAMBULIA ALAMA MOJA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 28, 2022

UJERUMANI WAAMBULIA ALAMA MOJA

 

Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya Ujerumani imepata alama moja pekee katika michezo miwili ya Kombe la Dunia 2022 inayoendelea nchini Qatar, baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya taifa ya Hispania kwenye dimba la Al Bayt.

Kwenye mchezo huo Hispania walipata bao lao kupitia kwa Mshambuliaji Alvaro Morata katika dakika ya 62’, huku bao la kusawazisha la Ujerumani likifungwa na Nicolas dakika ya 82’.

Msimamo wa Kundi E, Hispania wanaongoza msimamo wakiwa na alama nne, huku Japan na Costa Rica wote wakiwa na alama tatu, Ujerumani wana alama moja pekee.

Ujerumani, Hispania wamebakisha mchezo mmoja kila mmoja kumaliza mzunguko wa tatu wa Kundi E, Ujerumani watacheza dhidi ya Costa Rica huku, Hispania watacheza na Japan.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad