KAMPUNI Kinara ya mafuta, TotalEnergies Tanzania imeadhimisha toleo la nne la wiki ya huduma kwa wateja kwa kuingia makubaliano na mgahawa wa Royal Oven ambao umefunguliwa katika kituo cha TotalEnergies Bagamoyo road, Morocco jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo wa wiki ya huduma kwa wateja Mkurugenzi Mkuu wa
TotalEnergies Tanzania, Jean Francois Schoepp amesema wateja wao ni
kiungo muhimu katika kuendesha, kukuza na kuendeleza biashara pamoja na
kukidhi mahitaji ya wateja wao.
Amesema,
wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka 2022 imebeba kauli mbiu ya 'Pamoja
Kila Hatua ' huku msisitizo ukiwa si kwa huduma ya mafuta pekee bali
huduma nyinginezo ikiwemo bidhaa za vilainishi, huduma za kuosha
magari, maduka ya Bonjour na huduma kutoka Royal Oven Bakery.
Ameeleza
kuwa, Kampuni hiyo imekuwa ikiweka kipaumbele kwa wateja wao katika
kuhakikisha wanakidhi mahitaji yao kupitia huduma zinazotolewa na
TotalEnergies.
"Katika
wiki hii ya huduma kwa wateja Afrika, hapa Tanzania tunawakaribisha
wateja wetu kutembelea vituo vyetu kote nchini na kufurahia huduma
zinazotolewa na TotalEnergies na kufurahia ofa zinazotolewa pamoja na
kupokea maoni yenu yatakayoboresha huduma zetu zaidi." Amesema.
Katika
wiki hiyo ya huduma kwa wateja watakaopata huduma katika kituo cha
TotalEnergies Bagamoyo road watapata ofa ya kujipatia beef burger moja
bure wakununua bidhaa ya beef burger katika mgahawa Royal Oven.
Aidha
amesema kuwa TotalEnergies inaamini kuwa wiki ya huduma kwa wateja ni
zaidi ya kuisherehekea bali ni muhimu katika kupokea na kubadilishana
maoni na kuwahimiza wateja wao kutumia kurasa za mitandao ya kijamii ya
kampuni hiyo kutoa maoni yao ambayo yatafanyiwa kazi na kuboresha zaidi
huduma zitakazokidhi matarajio za wateja wao.
Pia ameupongeza mgawaha wa Royal Oven Bakery kwa kuichagua TotalEnergies na kushirikiana nao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Royal Oven Bakery Patrick Meme amesema
wamekuwa sehemu ya TotalEnergies kwa kufungua tawi katika kituo cha
Bagamoyo road, Morocco na wateja watapata huduma bora za bakery kuanzia
saa 12 asubuhi hadi saa nne usiku.
"Tunawaalika
wateja wetu kuja kufurahia wiki ya huduma kwa wateja pamoja na kampuni
kinara ya TotalEnergies hapa Bagamoyo road Morocco na kupata ofa katika
mgahawa pendwa wa Royal Oven." Amesema.
Mkurugenzi
Mkuu wa TotalEnergies Tanzania Jean Francois Schoepp akitoa huduma kwa
mmoja wa wateja waliofika kituoni hapo kupata huduma.
Mkurugenzi
Mkuu wa TotalEnergies Tanzania Jean Francois Schoepp akiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi na TotalEnergies na Royal Oven Bakery.
Muonekano wa Royal Oven Bakery katika kituo cha TotalEnergies Bagamoyo road, Morocco.
No comments:
Post a Comment