NYANGASA: IGENI MFANO WA MERIDIANBET - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 27, 2022

NYANGASA: IGENI MFANO WA MERIDIANBET

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Fatma Nyangasa ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kuiga mfano wa Kampuni ya Meridianbet Tanzania, ameyasema hayo wakati akiongoza zoezi la Usafi katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo kwa kushirikiana na Kampuni ya Meridianbet Tanzania kama vile maeneo ya kituo cha daladala cha Kivukoni Feri.


Katika zoezi hilo la kuweka mazingira safi Mkuu wa Wilaya Mh Fatma Nyangasa alitoa shukrani zake kwa kampuni ya Meridianbet kwa kutoa msaada wa vifaa vya kufanyia Usafi pamoja na maji ya kunywa pia na kwa kujitoa kwao kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo.

"Kampuni ya Meridianbet imekuwa mstari wa mbele kwenye kushiriki shughuli za kijamii, kama hili la leo, wameungana nasi kufanya usafi na kutupa msaada wa vifaa vya usafi, hivyo nawashukuru kwa kujitoa kwenu hiki mlichokifanya ni kikubwa sana, naomba muendelee kama hivi na kampuni zingine zipate kuiga mfano wenu"- Fatma Nyangasa.
Nae Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Meridianbet Tanzania, Matina Nkurlu alisema,

"Kampunia ya Meridianbet imefurahi kuungana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kwenye zoezi hilo la usafi, pia tumeguswa na siku hii ya leo hivyo tumetoa vifaa vya usafi kwahiyo tunafahamu umuhimu wa kuweka mazingira safi na salama.
"Meridianbet tumekuwa tukishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, kama vile kutoa misaada kwenye Hospitali nyingi, vituo vya polisi, kwahiyo tumeona itakuwa ni jambo jema kuja kutoa msaada hapa Kigamboni ili kujenga mahusiano ya karibu zaidi na Wananchi. Hivyo natoa wito kwa makampuni mengine kuiga jambo hili zuri kwa jamii"- Matina

Mwenyekiti wa Dalaladala eneo hilo la kituo Bw Ahmed Seif ameishukuru kampuni ya Meridianbet kwa kusaidia vifaa vya usafi na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi zima la kufanya usafi.

"Nawashukuru Meridianbet kwa kuungana nasi na kutusaidia vifaa vyanusafi eneo hili, ukweli ni kwamba mmekuwa na moyo wa kutoa kwa jamii, hivyo niwaombe kuendelea kusaidia jamii" Ahmed Seif Mwenyekiti wa Daladala.
Kampuni ya meridianbet inatoa huduma za michezo ya kubashiri na kasino mtandaoni, msimu huu wa michuano ya kombe la dunia wana machaguo special na ODDS kubwa na bomba, beti na kitochi au beti bila bando. Pia ukicheza kasino mtandaoni ule mchezo wa AVIATOR unaweza kujishindia zawadi ya Simu janja aina ya Samsung A23

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad