Benki
ya NMB imetoa msaada wa vifaa vya elimu katika shule tano za
halmashauri ya wilaya ya Kilosa na Mvomero vikiwa na thamani ya Sh. Mil
35 milioni ikiwa sehemu ya kupunguza changamoto za elimu mkoani
Morogoro.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mabati, mbao, misumari
na madawati kwa shule za sekondari Murrad Sadiq Sekondari, Mziha
Sekondari huku kwa shule za msingi ni Madizini, Mlali, Matongolo na
Mkwatani.
Wakizungumza wakati wa hafla iliyofanyika katika shule
hizo kwa nyakati tofauti, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Matongolo
wilaya ya Kilosa, Sifa Jonas alisema shule hiyo imepokea msaada wa
madawati 50 yenye thamani ya Sh.Mil 5 ambayo yatasaidia tatizo la
wanafunzi kukaa chini wakati wa masomo yao ya kila siku.
Sifa
alisema shule ya msingi Matongolo ina jumla ya wanafunzi 2379 wavulana
wakiwa 1155 na wasichana 1224 huku kukiwa na madawati 236 huku kukiwa
kukihitajika madawati 557.
Shule ya Sekondari Murrad Sadiq
Mvomero na shule ya Sekondari Mziha zimepokea vifaa vya kuezekea majengo
ya vyumba vya madarasa kila mmoja vyenye thamani ya Sh. Mil 5 ili
kukabiliana na wimbi la wanafunzi wataojiunga na kidato cha kwanza
Januari mwaka 2023.
Mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi
Madizini wilaya ya Mvomero, Najma Ally amesema shule yao inakabiliwa na
changamoto ya wanafunzi wengi kukaa chini na msaada huo wa madawati 50
vitasaidia kupunguza changamoto ya wao kukaa chini.
Meneja wa
Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema benki hiyo kwa mwaka huu
imetenga kiasi cha zaidi ya sh. Bilioni 2 kwa ajili ya kusaidiana na
serikali kutatua changamoto katika sekta ya elimu, Afya na yanapotokea
majanga.
Meneja
wa benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (kulia) akimkabidhi moja ya
madawati 50, Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Mvomero, Bruno Sangwe wakati
benki hiyo ilipotoa msaada wa vifaa vya elimu kwa shule za msingi na
sekondari nne zenye thamani ya sh Mil. 25 katika hafla iliyofanyika
shule ya msingi Madizini Turiani mkoani Morogoro. kushoto ni Mkuu wa
shule ya Madizini, Darini Nassoro.
No comments:
Post a Comment