HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 24, 2022

MKUTANO MKUU WA 36 WA DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI KKKT KUFANYIKA NOVEMBA 27-30


Msaidizi wa Askofu Mkuu wa KKKT Dar Es Salaam, Chediel Lwiza akifafanua jambo nkwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 24, 2022.
Msaidizi wa Askofu Mkuu wa KKKT Dar Es Salaam, Chediel Lwiza kushoto akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuutambulisha Mkutano Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya KKKT. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa 36, David Mngurumi.

DAYOSISI ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania, (KKKT) kufanya Mkutano mkuu wa 36 Novemba 27 hadi 30, 2022. ambao hufanyika kila baada ya Miaka miwili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 24, 2022 Msaidizi wa Askofu Mkuu wa KKKT Dar Es Salaam, Chediel Lwiza amesema kuwa Mkutano huo utafanyika katika Usharika wa Mbezi Beach Utajadili mambo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya Dayosisi hiyo.

Amesema kuwa pamoja na mambo mengine watajadili utekelezaji wa kazi zilizofanyika katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kujadili nini kifanyike miaka miwili ijayo kulingana na mikakati ya Dayosisi.

"Tutajadili maendeleo ya Dayosisi katika nyanja ya kuhubiri Injili na huduma za kijamii, huduma ya afya, Elimu, Makundi Maalumu na mwenendo wa hali ya Uchumi kwa Ujumla." Amesema Lwiza

Katika mkutano huo amesema kutakuwa na uchaguzi wa Wenyeviti wa halmashauri za Idara na bodi za vituo.

Aidha Mkutano huo Mkuu utaongozwa na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa ukiwa na wajumbe 424 ambapo kati yao ni Wachungaji wote wa Dayosisi hiyo, wawakilishi wa Mabaraza ya wazee kutoka Mashirika 97 na Mitaa 280.

Wajumbe wengine ni kutoka benki ya Maendeleo, Upendo Media, Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam (TUDARCO) na wadau kutoka taasisi nyingine za dayosisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad