HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 19, 2022

 MAFANIKIO YAMBEBA MNDOLWA, ATAJWA KUTETEA KITI CHAKE.


Hivi karibuni Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangaza majina nane (8) ya makada wake walioteuliwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ngazi ya Taifa.

Makada hao ni pamoja na msomi mbobezi katika masuala ya kihasibu na kifedha nchini CPA. Dkt. Edmund Bernard MNDOLWA ambaye ndiye Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa sasa, wengine ni Fadhili Rajabu MAGANYA, Bakari Nampenya KALEMBO, Said Mohamed MOHAMED (DIMWA), Mwanamanga Juma MWADUGA, Ally Maulid OTHMAN, Ali Khamis MASUDI na Hassan Haji ZAHARA.

Kampeni za uchaguzi ndani ya Jumuiya hiyo zimeshika kasi huku mpaka sasa hali ikionekana kuwa shwari kwa maana ya hakuna viashiria vya rushwa zaidi ya vita ya maneno toka kila pande kutambiana kushinda nafasi hiyo ambayo Mwenyekiti aliyopo sasa anapewa nafasi kubwa ya kutetea nafasi yake kwa sababu ya kuwazidi sifa, uzoefu na uwezo wa kiuongozi washindani wake.

Uongozi uliopo sasa unatajwa kujivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi chao cha miaka mitano ikiwemo kuirejesha hadhi na heshima ya jumuiya hiyo kwa kuimarisha utawala bora hali iliyopelekea kuimarika kwa usimamizi na uendeshaji wa shule za jumuiya hiyo kiasi cha kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa.

Mengine ni kurejesha mali zilizoporwa huko nyuma, kuondoa vitendo vya ufujaji na ubadhirifu wa mali za Jumuiya hiyo hali iliyowawezesha kujenga na kukamilisha ofisi zake za makao makuu Dodoma badala ya kuendelea kuishi ofisi za kupanga.

Tunatambua kwamba ni haki ya kila mgombea kuomba uongozi lakini suala la kuchagua na kuchaguliwa ni maamuzi ya wapigakura. Hivyo wanachama walio wengi wa Jumuiya hiyo wamewaasa wajumbe wanaokwenda kupiga kura kutumia haki yao hiyo kwa kuchagua kiongozi wa kuendelea kuifanya Jumuiya hiyo kuwa imara, yenye hadhi na heshima.

Uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo utafanyika tarehe 24-25 Novemba, 2022. Huku CCM ikiwakumbusha wagombea wote kuheshimu Kanuni za uchaguzi za CCM na misingi ya chama kwa kufanya siasa safi na kuzingatia maadili ya Chama wakati wote.


 


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad