Kishindo cha UWT Njombe, Mwenyekiti Scolastika Kevela atetea kiti chake sasa kuludi upya - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, November 17, 2022

Kishindo cha UWT Njombe, Mwenyekiti Scolastika Kevela atetea kiti chake sasa kuludi upya

 Njombe

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake (UWT) mkoa wa Njombe umemchagua Scolastika Kevela kuwa mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kura 242 kati ya kura 266.Scolastika Kevela ametetea kiti hicho mara baada ya kuwa mwenyekiti tangu alipochaguliwa March 2021 kutokana na aliyekuwa mwenyekiti kuwa diwani mjini Makambako.

Mara baada ya kuchaguliwa tena na kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyi Bi Kevela amesema.

“Sio kazi nyepesi lakini nimeshinda kwa kishindo,ninawashukuru wajumbe wa mkutano Mkuu wa mkoani wa Njombe kwa kunichagua lakini pia hata halmashauri kuu kwa kurudisha jina langu maana kuja kuwa mgombea ni mchakato ninashukuru kwa kuaminiwa”Scolastika Kevela Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe

Ameongeza kuwa “Ahadi yangu kwa UWT ni huduma zilizotukuka,tuna vipaumbele vinci kwa sasa ikiwemo kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha Sabuni ambapo kengo liko tayari na kilichobaki mwaka huu ni kufunga mashine ili uzalishaji uweze kuanza kwa ajili ya kukuza uchumi wa UWT”Scolastika Kevela Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe

Naye Katibu wa CCM mkoa wa Njombe Julius Peter ameagiza kuvunjwa kwa makundi yote yaliyokuwapo katika jumuiya ya wanawake UWT mkoa wa Njombe kabla ya kufanyika kwa uchaguzi ndani ya chama hicho na kwamba hivi sasa kinachotakiwa ni kuungana kufanyakazi.

Baadhi ya wanawake wa UWT akiwemo Esteria Mbwilo,Tumain Mtewa na Neema Mbanga wamesema wanamatumaini makubwa toka kwa Viongozi wao katika kuhakikisha maendeleo yanasonga.

Msimamizi wa uchaguzi huo Juma Sweda ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Makete amesema Wajumbe hao wamemchagua Scholastica Kevela kuwa mwenyekiti wao kwa kumpa zaidi ya kura 200.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad