HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 18, 2022

Doris Mollel Foundation yaanza maadhimisho ya Mtoto Njiti nchini Uganda

Katika kuadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani,leo November17,2022.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel ameitumia siku hiyo kwa kuungana na Serikali ya Uganda na wananchi wake katika hafla maalumu ya kuadhimisha siku hiyo, iliyofanyika kwenye viwanja Vya Kiwoko, Kampala, Uganda.
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Doris Mollel alisema atajitahidi kusaidia kuihamasisha Serikali ya Uganda kufanya mapitio ya sheria ya likizo ya uzazi kwa Wazazi wanaopata Watoto Njiti, huku akiahidi kufungua  Ofisi nyingine ya Taasisi ya Doris Mollel nchini Uganda ili kuwasaidia Watoto njiti.

yeye kama Balozi wa Watoto Njiti, ataendelea na kazi yake ya kuwasaidia Watoto Njiti kila sehemu anapopata nafasi ya kuwasemea.
Shughuli hiyo iliandaliwa na Wizara ya Afya nchini Uganda, ambayo imemuomba Doris Mollel kuwa ‘champion’ wa Watoto Njiti Uganda na amekubali kuifanya kazi hiyo.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad