BIRIANI FESTIVAL NA COCA-COLA AWAMU YA PILI KUFANYIKA DODOMA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 13, 2022

BIRIANI FESTIVAL NA COCA-COLA AWAMU YA PILI KUFANYIKA DODOMA

 

 Kampuni ya Coca-Cola Kwanza kupitia kampeni yake ya Biriani Friday na Coka ambayo ilianza rasmi mwaka jana na kuendelea mpaka sasa, ikiwa na lengo kubwa la kuendeleza utamaduni wa Misosi na Coca-Cola, ambapo huwa tunatembelea wadau wetu mbalimbali wanao jishughulisha na upikaji biriani kila Ijumaa kwa kuwaunga mkono na kuhakikisha tunawapatia wateja wao wote Coca-Cola ya baridi pale wapatapo Biriani kwenye migahawa yao, na kuwawezesha migahawa na vitendea kazi kama T-shirts, Aprons na mikeka ya kutumia Biriani inapoliwa. Kampeni Birian Friday na Coke mpaka sasa imeshafikia migahawa zaidi ya 50,kwa mikoa ya Dar-es salaam, Dodoma, Morogoro, Tanga, Mtwara, Zanzibar na Mbeya.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa kutangaza Tamasha hilo la Birian Friday na Coke, Meneja Biashara na Masoko Coca-Cola Kwanza Wahida Mbaraka alisema kuwa tamasha la Birian Festival na Coke awamu ya pili itafanyika Dodoma mnamo tarehe 26 Novemba mwaka huu.

‘Kwenye tamasha ili, tutawakutanisha kwa Pamoja wapishi wa Biriani wa mkoa huu na wateja wao, tamasha la mwaka huu litakuwa ni la kipekee kabisa na utofauti mkubwa, sababu tutaweza kupata Ladha pia ya vyakula vya asili vya Dodoma, Vionjo vingi vya kiasili ambavyo vinabeba utaifa wetu, na vile vile kuangalia mechi za Kombe la Dunia’, Mbaraka alisema.

Mbaraka aliongeza kuwa kutakuwa na Migahawa Zaidi ya 15, Michezo ya Watoto wetu, tukiburudishwa na Bendi ya Bushoke na Dj mkali Dj D-ommy Pamoja na burudani nyengine nyingi, na zawadi mbali mbali.

Kupitia jukwaa hili napeda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha watanzania wote, wapenzi na wadau wa biriani na Coca-Cola, Familia, Marafiki kuja kujionea na kushiriki kwenye utamaduni huu, Tanzania nchi yetu, Dodoma ndio makao makuu yetu, Biriani na Coca-Cola ndio chaguo letu na Mpira wa Kombe la dunia ndio raha yetu.Tarehe ni 26/11/22 ( Jumamosi), Mahali ni viwanja vya wajenzi Maili Mbili Dodoma,kuanzia saa nne asubuhi, aliongeza Mbaraka.
Meneja biashara na Masoko Coca-Cola Kwanza Wahida Mbaraka (kati kati) akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni wa wiki wakati akitangaza Tamasha la Birian Friday na Coke awamu ya pili ambalo litafanyika Dodoma mwishoni mwa mwezi huu. Lengo la tamasha la Birian Friday na Coke ni kuwakutanisha pamoja wapishi wa birian kwa kuendeleza utamanduni wa Msosi na Coca-Cola. Kulia ni Meneja wa Beni ya Bushoke Anileth Bushoke.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad